PIERRE Emerick Aubameyang, nahodha wa kikosi cha Arsenal ameiongoza timu yake kutwaa mataji mawili muhimu ikiwa ni lile la Kombe la FA pamoja na Ngao ya Jamii iliyochezwa usiku wa kuamkia leo kwa kushinda kwa penalti 5-4 mbele ya Liverpool.
Aubameyang raia wa Gabon amekuwa ni mhimili kwenye timu hiyo ambapo kwenye mchezo wa Kombe la FA alifunga mabao yote mawili, Agosti Mosi Uwanja wa Wembeley dakika ya 28 kwa penalti na dakika ya 67 huku lile la Chelsea likifungwa na Christain Pulisic dakika ya 5.
Mchezo wa usiku wa kuamkia leo Auba alitupia bao lake dakika ya 12 na liliwekwa usawa na Takumi Minamino dakika ya 73 lililowafanya wafikishane kwenye hatua ya matuta ambapo Arsenal ilishinda kwa mabao 5-4.
Nyota huyo amesema kuwa ni ushindi wa wote kwa kuwa walijipanga kuona namna gani wanaweza kupata ushindi jambo ambalo ni furaha kwa mashabiki na wachezaji kiujumla.
"Ni furaha kwetu na ilikuwa muhimu kushinda tulianza na FA kisha sasa tupo na Ngao ya Jamii hivyo hamna namna tunafurahi kuwa katika furaha hii," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment