WAKATI leo Jumapili Yanga wakiwa na kilele cha Wiki ya Mwananchi, ofi sa habari wa timu hiyo, Hassani Bumbuli amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Mkapa jijini Dar ili kushuhudia ufundi wa wachezaji wao na uimara wa jeshi lao kwa msimu wa 2020/21.
Yanga mpaka sasa imekamilisha usajili wa nyota 12 wapya ambao wanatarajiwa kutambulishwa rasmi mbele ya mashabiki leo ndani ya Uwanja wa Mkapa katika kilele cha Wiki ya Mwananchi.
Bumbuli alijinasibu kuwa, mandalizi yote kuelekea tukio hilo yamekamilika na kilichobaki ni kusubiri muda tu ili waandikishe rekodi mpya.
“Maandalizi yote kuelekea kilele cha Wiki ya Mwananchi yamekamilika kwa kiasi kikubwa na kilichobaki hivi sasa ni kusubiri tu muda ufi ke tuandike rekodi nyingine kubwa, tunaamini mashabiki watajitokeza kwa wingi kuja kuishuhudia Yanga mpya.
“Pamoja na burudani nyingine nyingi zitakazokuwepo, watu wajiandae kushuhudia ufundi mkubwa kutokana na usajili wa mafundi kama Mukoko Tonombe, Tuisila Kisinda na Carlos Stenio Fernandes Guimaraes do Carmo weyewe wanamuita Carlinhos,” alisema Bumbuli.
0 COMMENTS:
Post a Comment