UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa uwepo wa nyota wapya watano ndani ya kikosi hicho ni sababu ya timu hiyo kuanza maandalizi mapema kwa ajili ya msimu wa 2020/21.
Azam FC
imemalizana na nyota watano ambao ni viungo wanne Awesu Awesu,Ally
Niyonzima,Ayoub Lyanga,Isamail Kada na David Kissu ambaye ni kipa.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa
walianza maandalizi tangu Agosti 5 lengo ikiwa ni kuwafanya wachezaji waanze
kuzoeana mapema.
“Unajua
tumesajili wachezaji wengi kwa sasa ni lazima tuanze maandalizi mapema lengo
letu ni kuona kwamba wanazoeana mapema na kutengeneza muunganiko mzuri ambao
utatupa matokeo chanya.
“Tumeshamaliza
kusajili wachezaji watano malengo ilikuwa ni kuongeza nguvu kwa kusajili
wachezaji nane hivyo bado watatu ili tukamilishe mapendekezo ya mwalimu,
Aristica Cioaba,” amesema Thabit.
0 COMMENTS:
Post a Comment