August 23, 2020

 
IMERIPOTIWA kuwa Klabu ya Manchester United imekata tamaa ya kupata saini ya nyota, Jadon Sancho mpaka msimu ujao kwa kuwa hawapo tayari kukaa chini kujadili kuhusu bei ya kumpata mchezaji huyo.

Borussia Dortmund inayoshiriki Bundesliga wanahitaji pauni milioni 108 ikiwa ni ada ya kumpata mchezaji huyo huku mshahara wake ukitajwa kuwa pauni 300,000 kwa wiki kutokana na mfumo wa klabu ulivyo.

Kutokana na jambo hilo inaelezwa kuwa United inafikiria kujipanga kuipata saini ya nyota huyo mpaka mwaka ujao kutokana na dau hilo kuwa kubwa. 

Sancho amekuwa bora msimu uliopita akifunga jumla ya mabao 20 na kutoa pasi 20 kwenye mechi 44 ambazo amecheza jambo ambalo limemfanya gharama yake kuwa kubwa na United imekuwa ikiripotiwa kupambana kuipasta saini yake.

United inaamini kwamba mpangilio wa matumizi ya fedha uliyumba kidogo kutokana na janga la Corona  kwa kuwa masuala ya fedha hasa kwenye mauzo ya jezi pamoja na mambo mengine yaliyumba hivyo wanajipanga kumtafuta mbadala wake ambapo anatajwa Douglas Costa wa Juventus.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic