LEO Agosti 23, Uwanja wa Azam Complex ni kilele cha Azam Festival ambapo inatarajiwa kuchezwa mechi ya kirafiki kati ya kikosi cha Azam FC dhidi ya Namungo FC.
Kabla ya mechi hiyo kutakuwa na mechi nyingine za utangulizi ambazo zitachezwa ikiwa ni lengo la kutoa burudani kwa masbaiki wa Azam FC.
Malengo makubwa ya Azam FC ni kutambulisha wachezaji wapya kwa mashabiki pamoja na kutambulisha uzi mpya watakaotumia kwa msimu wa 2020/21.
Hawa hapa baadhi ya nyota wapya watakaotambulishwa leo Agosti 23:-Awesu Awesu (Kagera Sugar), Ally Niyonzima, (Rayorn Sports), Ayoub Lyanga,(Coastal Union),Ismail Kada,(Tanzania Prisons),David Kissu,(Gor Mahia),Emmanuel Charlse,(Mbao), Prince Dube (Highlanders FC).
Tunakutakieni kila la kheri Azam
ReplyDeletePoa
ReplyDelete