Morriosn aliibuka ndani ya Simba akitokea Klabu ya Yanga kwa dili la miaka miwili ambapo mechi yake ya kwanza ilikuwa jana, Agosti 22 Uwanja wa Mkapa mbele ya Vital'O ya Burundi.
Mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa ulikuwa na lengo la kutambulisha wachezaji wapya ndani ya Simba pamoja na kutambulisha jezi ambayo itatumika na Simba kwa msimu wa 2020/21.
Kwenye mchezo huo Simba ilishinda mabao 6-0 huku mfungaji wa bao la kwanza akiwa ni Morrison akimalizia kazi iliyofanywa na Larry Bwalya.
Alipofunga bao hilo Mrrison aliwachetua mashabiki wa Simba kwa mtindo wake wa ushangiliaji ambao aliwahi kufanya hivyo Machi 8 Uwanja wa Mkapa alipowatungua mabosi wake hao wakati huo akikipiga ndani ya Yanga.
Pia Morrison aliweza kumtengeneza nafasi ya kufunga nahodha John Bocco ambaye alifunga bao la pili na kumfanya aweze kutoa pia pasi kwenye mchezo wake wa kwanza ndani ya Simba .
Morrisons amesema kuwa anaipenda Simba ni chuo cha mpira ndani ya Tanzania.
Maneno kuntu
ReplyDeletekila mchezaji anapenda kuchezea simba
ReplyDelete