August 23, 2020

 KLABU ya Mtibwa Sugar yenye maskani yake Morogoro huku ikitumia Uwanja wa Gairo kwa mechi za nyumbani  ambazo hazina idadi kubwa ya mashabiki huku zile za Yanga na Simba zikipigwa Uwanja wa Jamhuri umekamilisha usajili wa wachezaji watatu.

Nyota wa kwanza kumalizana na Mtibwa Sugar alikuwa ni kiungo Abal Kassim Hamis ambaye amejiunga na klabu hiyo kwa mkopo akitokea Klabu ya Azam FC.

Wa pili alikuwa ni George Makang’a kutoka Namungo naye ni kiungo.

Mchezaji wa tatu ni Baraka Majogoro rasta aliyekuwa anakipiga ndani ya Polisi Tanzania naye pia ni kiungo.

Majogoro amesema kuwa anaamini msimu ujao utakuwa na ushindani mkubwa nao watapambana kufikia malengo ya timu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic