August 6, 2020

BEKI wa kati Abdallah Haji Shaibu 'Ninja' leo Agosti 6 amesaini dili la miaka miwili kuitumikia Klabu ya Yanga.

Ninja msimu wa 2017/18 alikuwa anakipiga ndani ya klabu hiyo alipata timu Serbia iliyokuwa inaitwa MFK Vyskov iliyomtoa kwa mkopo akacheze ndani ya Klabu ya LA Galaxy nchini Marekani.

Baadaye alirudi tena kwenye Klabu yake ya MFK Vyskov ambako alikosa nafasi ya kudumu kikosi cha kwanza jambo lililomfanya arejee nyumbani Tanzania.

Alianza majaribio ndani ya Yanga chini ya Luc Eymael aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga ambaye amefutwa kazi Julai 27 na hatimaye leo ametambulishwa rasmi kurejea kwenye timu yake ya zamani.

Huu unakuwa ni usajili wa tano kwa Yanga ambayo ipo kwenye mchakato wa kuboresha kikosi ikiwa imemalizana  na Bakari Mwamnyeto ambaye ni beki kutoka Coastal Union, Zawadi Mauya kiungo kutoka Kagera Sugar, Yasin Mustapha beki kutoka Polisi Tanzania na Wazir Jr mshambuliaji kutoka Mbao FC.

18 COMMENTS:

  1. Kwel nmeamua kubomoa timu sio kujenga timu kwa usajili huo

    ReplyDelete
  2. Utopolo bhana! Sasa huyo ana tofauti gani na Ally Ally mliyemtimua?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli wapenzi wa mikia mnadata safari hii,msipoangalia mimba zitawatoka,na kwa haya makombora laZima msajili wachezaji si chini ya Saba maana huu mkwara unawatoa shimoni

      Delete
    2. Ally Ally aliwahi hata kujaribiwa Uganda?

      Delete
  3. Nyie Manyani FC mnasajili kwa mihemko wakati ambapo Mikia FC wanasajili kwa umakini mkubwa

    ReplyDelete
  4. Mkwara wa kumsajili ninja. Hahahahahahahahahahhahahahahahshahahhs

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ame wa Coastal ni mchezaji wa kuvizia bandari ?
      Leo mmemkosa Mwamnyeto naona hata Magazeti Kama haya yanatia huruma poleni,eti Mwamnyeto si chaguo la Kocha wa Thiimba ni kweli hii???

      Delete
    2. Wakati tunamfunga coastal kwani Mwamnyeto hakuwepo

      Delete
    3. Sasa kisa cha kwenda kumvizia mchezaji wa Coastal bandarini nini kama Coastal mliifunga?
      Wanaoujua mpira hawajaacha kamwe kuwagombania wachezaji wa Brazil tena kwa gharama kubwa,ninawamaanisha wale wa kikosi cha timu ya taifa kilichopigwa 7-1 na Ujerumani

      Delete
    4. Tuliwafunga coastal bao nane yeye hakuwepi

      Delete
  5. Mikia fc mbona mnafoka hahaha maku....nyie

    ReplyDelete
  6. Kwa hakika bora timu ingebaki ile ile kuliko hawa wanaosajiliwa sasa.Mwakani tutapigania kutoshuka daraja na wala sio kuchukua ubingwa kwa aina hii ya usajili.Hata kama tuna dhiki lakini sio kwa usajili wa wachezaji type ya akina Ninja wa Kiembesamaki

    ReplyDelete
  7. Hivi ni kweli walitaka kuwasainisha mikataba mipya Yondani na Abdul bure bure bila hata bakshishi? Kama ni kweli sio fair. Labda kama kuna sababu zingine nyuma ya pazia

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mtaisoma namba ,kila usajili sasa hv mashine ya Jet
      Ulitaka tubaki na Molinga ufurahi,jiandaeni kuona udhaifu wa Wawa

      Delete
    2. Pole mikia inauma Sana ,kuona haya majaaa pamoja na kuyadanganya yamekata matawi yenu.hamyafungi tena hapa mtahitaji msaada was marefa tena

      Delete
    3. Msimu uliopita mlipiga sana kelele kuusifia usajili wenu ila nyinyi ninwa hapahapa manyani fc

      Delete
    4. Hafadhari sisi na Timu ya hapa hapa siyo ninyi mnajimwambafaia matokeo yake UD SONGO sisi angalau tulienda tukafia ICU lkn siyo mapokezi tena bila kupokelewa

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic