August 6, 2020


DAVID Kissu kipa aliyekuwa akikipiga Gor Mahia ya Kenya leo, Agosti 6 amefuzu vipimo vya afya kwa ajili ya kumalizana na mabosi wa Azam FC.

Kissu aliibukia Gor Mahia akitokea Klabu ya Singida United, amewahi kuitumikia Njombe Mji pia alikokuwa akikipiga na Ditram Nchimbi ambaye naye alikipiga Azam FC kisha akapelekwa Mwadui FC kwa mkopo msimu wa 2018/19  na Polisi Tanzania msimu wa 2019/20 na sasa yupo Yanga.

Pia kipa huyo alikuwa ana namba ndani ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars hivi karibuni kabla ya janga la Virusi vya Corona kuvurugavuruga mambo.

Inaelezwa kuwa amesaini dili la miaka miwili ndani ya Azam FC kuwa  mbadala wa Razack Abarola ambaye mkataba wake umeisha na kwa sasa yupo zake Ghana.

Anaungana na makipa wazawa ndani ya Azam FC ambao ni Mwadini Ally na Benedict Haule chini ya Kocha Mkuu, Arstica Cioaba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic