August 25, 2020

 


UONGOZI wa Azam FC, leo Agosti 25 umemalizana na makocha wake watatu wanaounda benchi la ufundi kwa ajili ya kuendelea kuwa ndani ya kikosi hicho kwa msimu wa 2020/21.

Makocha hao ambao wameongeza  mkataba leo ni pamoja na Kocha Mkuu Aristica Cioaba, raia wa Romania.

 Kocha Msaidizi, Bahati Vivier na Kocha wa Viungo, Costel Birsan, ambapo kila mmoja ameongeza mkataba wa mwaka mmoja.

Agosti 23, Azam FC waliwatambulisha wachezaji wake wapya pamoja na benchi la ufundi ambalo lilianza kazi kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Namung FC.

Kwenye mchezo huo uliohudhiuriwa na mashabiki wengi, Azam FC ilishinda mabao 2-1, Uwanja wa Azam Complex.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic