MRISHO Ngassa, kiungo mkongwe ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara aliyekuwa akikipiga Yanga msimu wa 2019/20 anatajwa kuingia kwenye rada za Gwambina FC na Ihefu ambazo zinahitaji kuboresha vikosi vyao.
Ngassa ameachwa na Yanga msimu huu wa 2019/20 baada ya mkataba wake kumalizika ndani ya Yanga na amepewa baraka za kuibukia timu yoyote atakayoiitaka kwa msimu wa 2020/21 na mabosi wake wa zamani wa Yanga.
Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa Ngassa zimeeleza kuwa tayari Gwambina ambayo imepanda Ligi Kuu Bara pamoja na Ihefu wao wana hesabu za kuipata saini ya Ngassa ili akaongeze uzoefu ndani ya Gwambina FC.
"Ameachwa na Yanga yupo huru kwa sasa na anaweza kuibukia ndani ya Gwambina kwani ana uwezo na kipaji kikubwa hivyo hatakosa namba kikosi cha kwanza ndani ya Namungo," ilieleza taarifa hiyo.
Ngassa amesema:"Bado kwa sasa sijaanza kufuatilia michongo kwani niponipo kwanza,".
Astaafu mpira huyo
ReplyDeleteDaaah saleh unakurupuka sana kuandika taarifa zako hazina weledi kabisa kusema kuwa anaweza kuibukia gwambina kwan ana uwezo na kipaji kikubwa hivyo hatakosa namba kikosi cha kwaza ndani ya namungo umemaanisha nn kuna uhusiano gan kati ya gwambina na namungo be care bro
ReplyDelete