August 1, 2020


INAELEZWA kuwa Klabu ya KMC imefikia makubaliano ya kumuachia nyota wao Charles Ilanfya kwenda Klabu ya Simba SC inayonolewa na Sven Vandenbroeck.

Mshambuliaji huyo mzawa ambaye amekuwa bora mwishoni mwa msimu baada ya kuanza kwa kusuasua kwa kuwa alikuwa anasumbuliwa na majeraha ya misuli ya nyama alikuwa kwenye rada za Yanga pia.

Aliibuka ndani ya KMC msimu wa 2018/19 akitokea Klabu ya Mwadui FC ambapo alivunja mkataba huko kutokana na ishu ya kutolipwa stahiki zake.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ilanfya amesema kuwa hana hiyana iwapo itatokea Simba ama Yanga zikahitaji saini yake kwa kuwa ni mchezaji.

"Sina presha na uwezo wangu ikitokea Simba ama Yanga wakahitaji saini yangu sina tatizo nitafanya kazi ila kwa sasa bado nipo ndani ya KMC," amesema.

Habari kutoka ndani ya KMC zinaeleza kuwa wamewaambia Simba kwamba iwapo wanahitaji saini ya nyota huyo ni suala la kukaa mezani.

7 COMMENTS:

  1. Simba inahitaji kusaini wachezaji wa viwango vya juu sana sio mchezaji wa kawaidakawaida viongozi msifanye makosa hayo.

    ReplyDelete
  2. Hao wachezaji wenu wa ndondo cup hatuwahitaji tafadhalini sana kama hamuwezi kusajiri bora muwache wenzetu wameshaanza na tumeona sisi mnataka mtuletee hao karagosi wenu tafadhali

    ReplyDelete
  3. Tunataraji sana kimya cha Mnyama Bila ya kubweka ovyoovyo kina mshindo mkubwa Sana kutawafanya wengi kupiga magoti na kulia mateka kabla ya boli kuwekwa chini

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic