MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga,Yacouba Sogne raia wa Burkina Faso anatarajiwa kutua nchini leo Agosti 31, akitokea nchini Burkina Faso.
Nyota huyo ilibidi atue nchini Agosti 27 na mashabiki wa Yanga walijitokeza kwa wingi Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere (JINA) ila alishindwa kutua na alikosa tamasha la Wananchi lililofanyika jana Uwanja wa Mkapa ambapo wachezaji wapya na jezi mpya ya Yanga kwa msimu wa 2020/21 ilitambulishwa.
Yacouba alimalizana na Yanga kwa dili la miaka miwili akitokea Asante Kotoko ya Ghana mara baada ya mkataba wake kuisha na anakuja akiwa ni mchezaji huru.
Kwa mujibu wa Mjumbe wa Kamati ya Usajili Yanga na Mkurugenzi Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said alisema kuwa ndege yake ilizuiliwa kutua nchini hivyo amekatiwa tiketi nyingine na atatoka kwao Burkina Faso Agosti 30.
Hersi alisema kuwa mshambuliaji huyo baada ya kutua nchini, ataungana na kambi ya pamoja kwa ajili ya kuanza mazoezi ya pamoja kujiandaa na msimu mpya wa ligi na tayari wachezaji wa Yanga walianza mazoezi Agosti 10.
“Agosti 31 atawasili nchini na hatakuwepo kwenye kilele cha Tamasha la Wiki ya Mwananchi,” alisema Injinia.
Onfeza magarasa mwanangu...,.niebdelee kukupigia mabao kila siku
ReplyDeleteOngeza magarasa mwanangu.... niendelee kukupiga mabao kila siku
ReplyDeleteEndelea kuota chooni!
ReplyDeleteMikia fc,cjui mnawaza kutumia nini! Ndoto za njiani zitawaponza
ReplyDeleteHaya ndio Songe ndio anafika, haraka kimbilieni eyapot Gongowazi mkampokee msiondoke mpaka afike kunyanyua molali ikiwezekana angalau muonje ushindi angalau wa kikombe cha Kahawa baada ya ukame ulioingia msimu wa nne
ReplyDelete