August 25, 2020

 


KMC FC leo Agosti 25 imekamilisha usajili wa golikipa kutoka Mbao FC, Raheem Sheikh kwa mkataba wa miaka miwili.


Nyota huyo mikono mia anaungana na nyota wenzake 9 na kufanya KMC iwe imesajili jumla ya nyota 10 mpaka sasa kwenye dirisha la usajili lililofunguliwa Agosti Mosi na linatarajiwa kufungwa Agosti 31.

Wengine ambao nao wameshamalizana na Klabu ya KMC yenye maskani yake Kinondoni ni pamoja na:-.

Agosti 24, ilimalizana na nyota kutoka Lipuli FC, Kenneth Masumbuko kwa kandarasi ya mwaka mmoja.

Agosti 23 ilimalizana na Reliants Lusajo mtupiaji kutoka Namungo FC kwa dili la mwaka mmoja akiwa mchezaji huru.

 Agosti 20, ilimalizana na David Brayson beki wa kushoto kutoka Gwambina FC kwa kandarasi ya mwaka mmoja na beki wa kati Lusajo Mwaikenda kutoka Azam FC kwa mkopo wa mwaka mmoja pamoja na beki Israel Patick kutoka Alliance naye pia dili la mwaka mmoja.

Agosti 19 ilimalizana na kiungo mkabaji Masoud Abdalah kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Azam FC. 

Mwingine aliyetambulishwa Agosti 19 ni kiungo mshambuliaji Martin Kigi kutoka Klabu ya Alliance FC kwa dili la mwaka mmoja.

David Mwasa kutoka Lipuli beki kwa kandarasi ya miaka miwili na usajili wa kwanza kutambulishwa ulikuwa ni kwa Andrew Vincent,'Dante' Agosti 18 alikuwa anakipiga Yanga kwa dili la mwaka mmoja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic