August 22, 2020


 MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Nasib Abdul, Diamod leo Agosti 22 ameweka rekodi yake kwa kutumbuiza mbele ya mashabiki wa Simba ambao walijitokeza kwa wingi Uwanja wa Mkapa kwenye kilele cha Simba day.


Diamond alitua Uwanja wa Mkapa akiambatana na Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kwa Helkopta jambo lililozua shangwe kwa mashabiki mwanzo mwisho.


Baada ya kushuka Mondi alianza kutoa burudani moja kwa moja bila kusubiri kuitwa na MC Mpoki kama ilivyokuwa kwa Meja Kunta na  Mario ambao nao walitumbuiza kwenye tamasha hilo.


Wimbo mpya wa Simba aliurudia mara mbili huku mashabiki wakimshangilia nyota huyo mwenye uwezo wa kuimba na kucheza.


Katika harakati za kucheza Mondi, shabiki mmoja ambaye hakufahamika jina lake alimrukia Mondi na kumkubatia jambo lililozua tafrani kidogo kabla ya shabiki huyo kuondolewa na Polisi pamoja na mabausa wa Mondi.


Licha ya Mondi naye kuanguka alijifuta na kuendelea kupiga show baada ya kumaliza alisepa kwa kukwea Helkopta na kumuacha Manara akiendelea na shughuli za kuwatambulisha wachezaji wapya na wazamani wa Simba kwenye kilele cha Simba day.

 Inaelezwa kuwa 'Surprise' ambayo ilikuwa ikisemwa na Manara awali kabla ya kilele cha Simba day ilikuwa ni burudani kwa mashabiki wake kutoka kwa wasanii wa Bongo pamoja mtindo wa kutoa kwa Manara na Mondi kwa kutumia Helkopta.

10 COMMENTS:

  1. Waige na wao utopolo mambo adimu kutoka kwa mnyama

    ReplyDelete
    Replies
    1. Jamani mnaamini kweli Suprise yenyewe ni Helicopter? watanzania wa karne hii? Mo sisi tunasubiri Suprise uliyotuahidi sisi sio watoto wa kutudanganya kwa Chopper.

      Delete
  2. Kuiga kwao Kuna mpaka lakini hii ni juu ya uwezo wao na kwa wakati huu kinachowshughulisha zaidi ni kumshugulikia Morrison hasa walivouona uwezo wake na matamshi ya kukata moyo pale alipojielezea furaha yake uwepo wake Simba na alipojielezea hiyo timu yake mpya

    ReplyDelete
  3. Jamani uma wote ule ni wa Simba. Ilikuwa kila pahali wekundu tu weupe wala wa njano hsukuonekana. Yajana tumeyaona tunangoja yanayokuja, yatanoga kama alivonogesha Manara na Moo mwenyewe na Mondi?

    ReplyDelete
  4. Kwa wapambanuzi wa mambo kwa kilichoonekana ktk wiki hii kwa mabadiliko ya Mo ya kujitwishwa kazi ya Manara, ni dhahiri tunatakiwa kumpa Big Up Rais wetu. Tunaweza kusema Heshima imerudi Tz. Watu wapate wanachostahili kulingana na jasho Lao. Hii hakika haijawahi kutokea. Tajiri anajitetea kushindwa kulipa fedha alizonunulia timu! Mikia hiyo ni tahadhali kwenu.

    ReplyDelete
  5. Mtu mnafiki utamjua tu, roho sitawauma sana. This is simba brother another level badala ya kutengeneza timu ilete ushindani mnaomba Mungu kila siku Mo ata angekufa ili simba ianguke, Simba sio mo brother, simba ni kubwa zaidi ya mo, mo ataondoka simba ataicha itabaki, na anaweza kuja mtu mwingine vilele ambaye amumzaanii akaja kuwekeza zaidi ya mo maisha ndivyo yalivyo vumilieni vumilieni labda kama baada ya miaka 6 manweza mkaanza kutuchalenji

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unafiki? Wewe inaonekana huelewi chochote? Hiyo timu ni mali ya Mo. Wewe ni shabiki wake. LOGO ya timu kashabadili. Kama hamjui hilo basi tatizo kubwa zaidi.

      Delete
    2. Ni unafiki tena una wivu wa kike.Wewe ni sawa na mbuzi anayepigiwa zumari na hata Luc Eymael hakukosea kuwambia yale maneno.Simba inajenga taasisi ambayo hata MO akiondoka na hisa zake 49% bado wanachama wana hisa zao 51% na hata serikali inajua hilo na MO ameshawaambia haondoki Simba na wana Simba wanamuelewa sana na sio wale jamaa wa mlima Kitonga.

      Delete
    3. Watarithi watoto wake kama hujui. Amebadili logo nyie wanachama wenye 51% mmeshirikishwa? Kasome tena capital structure and control of company. Mo ana 49% je anayefuatia kwa wingi wa share ni nani? Yani kweli Mikia wote mnategemea akili za Manara tu?

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic