Mchezo wa leo ulikuwa na lengo la kutambulisha wachezaji wapya pamoja na jezi itakayotumika kwa msimu wa 2020/21.
Ushindani ulikuwa mkubwa kipindi cha kwanza ambapo iliwabidi Simba wasubiri mpaka dakika ya 43 kupata bao la kwanza kupitia kwa Bernard Morrison ambaye alimaliza kazi ya pasi ndefu ya Larry Bwalya ambaye naye ni nyota mpya wa Simba.
Dakika mbili mbele, Morrison alitengeneza pasi kwa nahodha wa Simba John Bocco ambaye alipachika bao la pili dakika ya 45.
Simba ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0 huku Vital'O ikiwa haijaambulia bao ndani ya dakika 45.
Kipindi cha pili, Simba ilifanya mabadiliko kwa wachezaji wake wote ambao walianza kikosi cha kwanza ambao ni Aishi Manula, Shomari Kapombe,Gadiel Michael,Ibrahim Ame,Joash Onyango,Jonas Mkude,Hassan Dilunga,Rarry Bwalya,John Bocco,Said Ndemla na Morrison.
Nyota walioingia ilikuwa ni pamoja na Beno Kakolanya ambaye aliumia dakika ya 64 na kumpisha Ally Salim, Mohamed Hussein,Keneddy Juma,Erasto Nyoni,Gerson Fraga,Mzamiru Yassin,Ibrahim Ajibu,Clatous Chama,Cris Mugalu, Charlse Ilanfya na Miraj Athuman.
Kikosi cha pili kilipachika mabao manne ambapo bao la tatu lilipachikwa na Chama dakika ya 56 akimalizia pasi ndefu ya Ajibu ambaye alifunga bao la nne dakika ya 75 kwa pasi ya Chama kisha bao la tano likapachikwa na Mugalu dakika ya 77 kwa pasi ya Miraj huku msumari wa mwisho ukipachikwa na Ilanfya kwa pasi ya Mohamed Hussein.
Sven amesema kuwa ulikuwa ni mchezo mgumu na mzuri huku wachezaji wake wakionyesha kile ambacho amewafundisha jambo ambalo linampa picha ya kikosi chake kuanza kufanya vizuri ndani ya ligi na mashindano mengine.
Kwa goli hiz, hii sio mechi ya kirafiki Tena, kuanzia lini rafik yako kweli umpe kipigo kizito hivi? Pia, kwa nini mikia huwa mnachukua timu mbovu??
ReplyDeleteKumbe hata aliyepigwa 4 ni mbovu
DeleteHata huyo alipigwa 4G in mbovu
DeleteWakitaka wasitake lakini wajuwe kuwa Mnyama anapiga hodi huyo na wenye kejeli, makelele,malalamiko yasiyokwisha na mbwembe nyingi bila ya kujifahamu wanachokitaka wajirekebishe au wataadhirika viba kwani siku nzuri Huanzia asubuhi
ReplyDeleteMabao kibao tu ajae mbele yetu akiwemo utopolo
ReplyDeleteHuko mitaani Gongowazi kimya na wamejiinamia na mara mojamoja humtaja Morrison na kusema bado mchezaji wao
ReplyDelete