August 24, 2020

 


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa una wachezaji wawili wazuri wa kimataifa ambao tayari umeshazungumza nao ila unapenda kurejesha usajili wao mikononi mwa mashabiki ili waweze kuwasijili wachezaji hao.


Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla amesema kuwa wana imani na mashabiki na wadau wa timu hiyo hasa katika masuala ya kujitolea kwa ajili ya timu yao hivyo wanaamini watafanikisha bila matatizo.

"Tunawachezaji wa kimataifa wawili ambao tayari tumeshazungumza nao kila kitu, ila tunaomba hawa gharama za usajili zifanywe na mashabiki na wadau ambao wamekuwa nasi kila wakati.


"Uwezo ninajua upo kwa sababu msimu uliopita walisajili wachezaji 10 mashabiki wenyewe ila msimu huu tunaomba waweze kusajili wachezaji wawili tu na utaratibu utatolewa hivi karibuni," amesema.

8 COMMENTS:

  1. Wakisajiliwa hao wachezaji wawili itafanya jumla ya wachezaji wa kigeni kuwa 11 kufuatana na orodha iliyotolewa na Yanga

    ReplyDelete
  2. Naona tunarejea yale ya Zahera mapema kweupe Bila ya kutegemea kuanza kuzungusha bakuli wakati wakati ikiaminika mabilioni yameshatumika kusajili kikosi kipya na kuahidi mengi zaidi, vipi tuseme ndio mfuko umekauka gafula wakati ambapo hata mambo hayajaanza. Ndio inabashiri nini au ndio mbio za sakafuni hizo? Haki ya Mungu lazima tukubali tunaumia pale wenzetu wanapiga hatuwa mbele sisi tunapiga hatuwa kumi nyuma. Ndio tuseme tuna rejea yale ya zamani.

    ReplyDelete
  3. Ikiwa ni hivo vipi itakuwa mishara au bakuli ndio litakizi kila kitu. Inashtuwa sana

    ReplyDelete
  4. Tupo tayari, YANGA NI YETU, popote ilipo tupo. Umoja Ni nguvu. DAIMA mbele YANGA yetu ndio MWANANCHI wetu.

    ReplyDelete
  5. Timu ni yetu, tutaiendesha wenyewe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic