August 24, 2020

 


WAZIRI wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni, Harisson Mwakyembe amesema kuwa Klabu ya Azam FC imeongeza thamani ya soka nchini na kujitengenezea nafasi ya kuwa timu kubwa na bora nchini.


Maneno hayo aliyasema jana Agosti 23, kwenye kilele cha Azam Festival makao makuu ya Azam FC, Chamazi.


Mwakyembe alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye alikuwa na udhuru.

"Serikali ambapo huwa inakwama kwenye masuala ya kimichezo ikiwa ni pamoja na uwanja huwa inakimbilia huku kwa Azam kwa kuwa mmejipambanua na kuwa bora katika miundombinu pamoja na kuwa na timu bora.


"Pia ni timu ambayo ina academy yake pamoja na miundombinu bora, kwa tamasha ambalo mmelifanya limeongeza thamani ya timu yenu na ninaamini kuwa mtazidi kuwa bora," amesema.


Burudani zilitolewa kwa mashabiki jana ikiwa ni pamoja na mechi za utangulizi, show kali kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba pamoja na msanii wa Singeli, Msaga Sumu.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic