Mchezaji Bora Chipukizi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu uliopita, Novatus Dismas, ameongeza mkataba mpya wa miaka miwili zaidi kuendelea kusalia Azam FC.
Dismas alikuwa anakipiga ndani ya Klabu ya Biashara United FC kwa mkopo msimu wa 2019/20.
Kiungo huyo mkabaji aliye kwenye kiwango bora, ataendelea kusalia katika viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2023.
0 COMMENTS:
Post a Comment