August 27, 2020


 IMERIPOTIWA  kwamba baba mzazi wa Lionel Messi, mzee Jorge Messi, amewasili katika jiji la Manchester kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kufanya mazungumzo na Klabu ya Man City juu ya uhamisho wa mwanaye, Messi,  ambaye ameshaomba kuihama Barcelona.

Messi anaripotiwa kuvutiwa zaidi na Man City ili kuungana tena na kocha wake wa zamani, Pep Guardiola. Messi ameshatangaza kuwa yuko huru kuondoka Camp Nou, kitendo ambacho kimefanya mashabiki kuandamana kushinikiza  klabu hiyo isimruhusu kuondoka.


Manchester City anapewa alama 5/2 kumnunua staa huyo wa timu ya Taifa ya Argentina.


Kwa mujibu wa Ripoti ya RAC1 na TyC Sports vimeeleza kuwa kuna mazungumzo ya Messi kujiunga na City kwa mkataba wa miaka miwili japo bado ni tetesi na hazijawekwa wazi na iwapo atalipwa uhamisho kwa sababu yeye ndiye ameomba kuondoka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic