August 13, 2020


 UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa kwa sasa hauna presha ya kuingia sokoni kufanya usajili kwa kuwa wanasubiri vurugu za Simba na Yanga ziishe sokoni kisha wao watafanya mambo yao.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa wanatambua kuwa kuna masuala ya usajili ila wanasubiri kidogo hali itulie ndipo waingie sokoni.

“Unajua Mtibwa Sugar ni shamba la vipaji sasa huwezi kuingia sokoni ukiwa haujui nani ataondoka na nani atabaki, tunasubiri vurugu za Simba na Yanga ziishe kisha tukishajua tunamapungufu wapi ndipo tutasajili.

“Ipo wazi ni lazima tufanye usajili kwani tulikuwa na msimu mbayambaya kuliko yote msimu huu, yale mapungufu tutayafanyia kazi ili tuwe imara msimu wa 2020/21.” Amesema Kifaru.

Mtibwa Sugar, msimu wa 2019/20  iliishia nafasi ya 14 ikiwa na pointi 45 baada ya kucheza mechi 38 ikiwa ni mara ya kwanza kuishika nafasi hiyo kwa muda wa misimu 10 mfululizo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic