August 6, 2020


KAMPUNI ya GSM iliyochukua jukumu la usajili Yanga kwenye msimu ujao, imemuwekea kitita cha Sh 50Mil, beki wa pembeni wa Nkana Rangers ya Zambia, Hassan Kessy.

Beki huyo ni kati ya wachezaji wanaowaniwa na Yanga katika kuiimarisha safu ya ulinzi ya kulia pamoja na beki wa KMC, Kelvin Kijiri ambaye klabu yake inahitaji Sh 60Mil ili imuachie kutokana na kubakisha mwaka mmoja katika mkataba wake.

Yanga hivi sasa ipo kwenye mipango ya kukisuka kikosi chao baada ya kutangaza kuachana na wachezaji wake 14 wakiwemo mastaa Papy Tshishimbi, David Molinga, Mrisho Ngassa na Issa Mohammed ‘Banka’.

Taarifa zinaeleza kuwa uongozi wa Yanga kwa kushirikiana na GSM walimuita beki huyo Jumapili usiku na kukaa naye mezani kwa ajili ya kufanya mazungumzo ambayo yalishindwa kufikia sehemu mzuri kutokana na dau kubwa ambalo amelitaka

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa beki huyo ametaka kitita cha Sh 60Mil kabla ya kupunguza kufikia Sh 55Mil kabla ya viongozi hao kumuwekea dau hilo la 50Mil pekee.

Aliongeza kuwa mabosi hao wamefikia makubaliano ya kumpa Sh 50Mil na mshahara wa Sh 4Mil, ambao nao ameukataa akitaka Sh 6Mil ya mshahara ili asaini.

“Bado muafaka mzuri haujafikia kati ya uongozi wa Yanga na Kessy aliyekuwepo kwenye mipango mizuri ya kurejea tena Jangwani baada ya mkataba wake Nkana kumalizika.

“Kikubwa walichoshindwana ni dau la usajili na mshahara pekee lakini mambo mengine kila kitu kinakwenda vizuri, upo uwezekano mkubwa wa beki na uongozi kumalizana ndani ya wiki hii," alisema mtoa taarifa.

Alipotafutwa Kessy kuzungumzia hilo alisema kuwa “Nipo kwenye mazungumzo mazuri na Yanga kama mambo yakienda vizuri nitasaini mkataba, nisingependa kuweka wazi dau la usajili ambalo mimi nilitaka kwani hiyo ni siri yangu na klabu.”

Chanzo:Championi

5 COMMENTS:

  1. Sasa kuliko kulipa milion 50 kumsajili Messy, si watoe hizo pesa kwa Yondani na Juma Abdul? Naamini Abdul yuko vizuri zaidi ya Kessy

    ReplyDelete
  2. Nakubaliana na wewe. Kessy kwanza haaminiki. Ana kahistoria.Viongozi badala ya kulipa uaminifu wa Abdul na Yondani wanambembeleza Kessy. Inashangaza.

    ReplyDelete
  3. Hii inashangaza sana, unawezaje ukamwacha Juma Abduli mchezaji mwenye mapenzi na Yanga ukabembeleze Kessy!? Kwanza kiuchezaji Kessy hawezi mfikia Juma Abduli, vilevile nani asiyejua Kessy ni Simba dam dam, huyu atakuja kutusumbua Yanga...kwa nini viongozi hawataki kujifunza kwa kina Morrison!?

    ReplyDelete
  4. Mnamwacha Tshishimbi mnaenda kubembeleza Kessy hilo Galasa, Nkana wameliacha kwasababu limekwisha....acheni uzembe Yanga. Sajilini wachezaji wenye maana wa kuisaidia Yanga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic