Messi mwenye miaka 33 amekuwa kwenye hesabu za kuondoka ndani ya Barcelona baada ya timu yake kupokea kichapo cha mabao 8-2 mbele ya Bayern Munich kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Ronaldo anaamini kwamba Barcelona ina nafasi ya kufanya vizuri kwa wakati ujao ila inaweza kuyumba kidogo ikiwa itamruhusu Messi aondoke ndani ya kikosi hicho.
Kipigo hicho cha udhalilishaji kilimfanya Messi amshushie lawama rais wa timu hiyo Josep Bartomeu kwa kudai kuwa ana maamuzi mabovu yanayoiyumbisha timu hiyo.
Ronaldo alicheza ndani ya Barcelona mwaka 1996-97 bado anaamni kuwa Messi anahitajika ndani ya Barcelona.
'Messi ni mchezaji muhimu ndani ya Barcelona kwa sasa kama ningekuwa ndani ya Barcelona nisingemuacha aondoke kwa kesi yoyote ile ambayo ingetokea.
"Amekuwa mchezaji mkubwa na mwenye mafanikio ndani ya timu, mahusiano yake na wachezaji wenzake ni mazuri ninaona kwamba bado Messi anahitajika ndani ya klbu hiyo ili kushirikiana na wachezaji wenzake," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment