September 8, 2020


RAIS wa Shirikisho la Soka Afrika, Ahmad Ahmad amemwandikia barua kumpongeza Mtendaji Mkuu (CEO) mpya wa simba, Barbara Gonzalez kwa uteuzi wake akimtakia kila la kheri katika majukumu hayo mapya.


Barbara Gonzalez ni CEO wa kwanza mwanamke kuteuliwa katika klabu za Ligi Kuu Tanzania jambo ambalo limemgusa Rais huyo wa CAF.


Barbara anachukua mikoba ya aliyekuwa CEO wa timu ya Simba, Senzo Mbata ambaye alijiuzulu hivi karibuni na muda mfupi tu picha zilisambaa akiwa na viongozi wa Yanga ambao kwa sasa wamempa dili akiwa ni mshauri mkuu wa klabu hiyo yenye maskani yake pale Jangwani.

Kupitia barua ya pongezi Rais amendika kuwa ni furaha kwake kuona nafasi kubwa ya uongozi kwenye masuala ya michezo akipewa mwanamke jambo linaloweka usawa katika kazi na usawa kwa jinsia.


Pia ameongeza kuwa anakubali uwezo wa CEO mpya na kumtakia kila la kheri katika utendaji wake wa kazi.


Pia CEO huyo alipewa pongezi na Ubalozi wa Marekani wa Tanzania huku ukieleza kuwa umekuwa ukiunga kwa muda mrefu masuala ya wanawake katika uongozi na ndani ya uwanja.

12 COMMENTS:

  1. Duuh, CAF wana upendeleo kwa Simba. Mbona hawakumwandikia barua Senzo Mbatha Mazingisa alipojiunga Yanga?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Senzo ni mshauri tu siyo CEO

      Delete
    2. Ndo mjue mumechukua MTU ambae sio wa umuhimu CAF

      Delete
  2. Kwanza Yanga haijulikan kimataifa kama Simba.

    ReplyDelete
  3. Kwanza Yanga haijulikan kimataifa kama Simba.

    ReplyDelete
  4. Kwanza Yanga haijulikan kimataifa kama Simba.

    ReplyDelete
  5. Mwisho niubalozi wake pia haujampongeza kuhamia yanga wajue simba next level Africa

    ReplyDelete
  6. Tukubali tu kuwa simba ni wazee wa ubunifu na mambo mengi wanayobuni yanamshiko yaani kisasa zaidi.Simba ilipatia kwa gonzale na ndio maana wanaume wasiojiamini wanatetemeka. Kitendo cha simba kumteua Barbara Gonzale kuwa CEO wao tayari kishaanza kuwanyima raha yanga. Kwanini? Yanga kwa siku za mbele itabidi waige tu kama wataamua kuajiri mwanadada kwa nafasi ya CEO.Ila kama CAF na jumuiya za kimataifa wanaipongeza simba kwa kuteua mwanamama kwa nafasi kubwa kama CEO wa timu,sisi hapa kwetu kiongozi fulani wa umma anaponda. Yawezekana pia Babra akahamasisha akina mama kufuatilia na kulipenda soka zaidi. Kwa wenye maono ya ndani uteuzi wa Babra kuwa CEO wa simba upo positive zaidi kuliko negative na itaitangaza simba zaidi ndani na nje ya nchi.

    ReplyDelete
  7. Kutokana na hayo, tunamtaka yule aliemtaka Moo kusepa a Rais WA Shirikisho LA Soka Africa na kuirejesha Simba Katika ile hali ya unyonge amsute

    ReplyDelete
  8. Hivi ile barua ya kutoka FIFA ya kuitaka Yanga ibadilishwe kutoka sport Club kwenda FC iliishia wapi? Kila wakati Wanatuletea habari za kujitungia tu

    ReplyDelete
  9. Hivi ile barua ya kutoka FIFA ya kuitaka Yanga ibadilishwe kutoka sport Club kwenda FC iliishia wapi? Kila wakati Wanatuletea habari za kujitungia tu

    ReplyDelete
  10. Simba Ni Simba, tushawahi kuwa na msemaji mwanamke na CEO tunapanda, hatubagui jinsia tunaangalia uwezo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic