UONGOZI wa Geita Gold, unatarajia kuandaa tamasha la kuwatambulisha wachezaji wapya waliosajiliwa katika timu hiyo tayari kuingia kwenye vita ya kupigania kupanda daraja msimu wa 2020/2021.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Katibu Mkuu wa Geita Fadhil Hassan, alisema tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Septemba 15, mwaka huu mkoani hapo.
Hassan alieleza mara baada ya kuyaanika wachezaji wapya wa msimu mpya, wataanza na mechi ya kirafiki na timu moja ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo bado wako kwenye mazungumzo ya kuipata.
“Tunaendelea na maandalizi ya kucheza mchezo wetu wa kutambulisha majembe yetu mapya. Tupo kwenye mazungumzo na timu mojawapo ya ligi Kuu na mazungumzo yanaendelea vizuri katika kuhakikisha mambo yanakuwa sawa,” alisema Fadhili.
Geita Gold inajiandaa na msimu mpya wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) 2020/ 2021, ikiwa inasubiri ratiba rasmi kutoka Bodi ya Ligi.
0 COMMENTS:
Post a Comment