KIPINDI cha
usajili kimemalizika na timu za Ligi Kuu Bara zilifanya usajili kuanzia Agosti Mosi
hadi Agosti 31, mwaka huu.
Baada ya hapo,
ligi ikaanza wikiendi iliyopita na wiki hii kipute kinaendelea kama kawaida ikiwa
ni raundi ya pili.
Kabla sijaenda
mbali sana, nitoe pongezi kwa klabu ambazo zilifanikiwa kufanya usajili kulingana
na mahitaji ya timu zao na sasa nyota hao wanatarajiwa kufanya makubwa.
Usajili ulipofanyika
tuliona timu zikipambana kujiimarisha hasa zile ambazo zilipanda daraja kwa upande
wa Ligi Kuu Bara ambazo ni Ihefu, Gwambina na Dodoma Jiji.
Ubora wa wachezaji
ambao waliwasajili kwenye usajili huu, tunaamini kabisa matunda yataonekana katika
msimu huu wa 2020/21, kutokana na baadhi ya timu kufanya mabadiliko makubwa kwenye
vikosi vyao kwa asilimia 80 mfano mzuri Yanga.
Pamoja na klabu
kufanya usajili huo bora lakini pia wanatakiwa kuzingatia pia ubora na nafasi za
wachezaji wa ndani kupewa nafasi kwa ajili ya maandalizi ya timu yetu ya taifa ambayo
ina michuano mbeleni ya kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika.
Hivyo ni vizuri
kwa timu zile ambazo zina wachezaji wa kigeni kuangalia kwa umakini kwa wachezaji
wazawa kupewa nafasi kuonyesha ubora kwa maslahi ya taifa letu kuhakikisha tunapata
nafasi ya kushiriki michuano hiyo mwakani.
Lakini hilo lisiwe
chachu ya kuwadumaza wazawa, mnatakiwa kujituma kwa nguvu zenu zote, ndipo mpate
nafasi.
Mnaweza kupewa nafasi kisha mkazifelisha timuzenu.
Nikiigusia mada
husika, tumeona wachezaji walipocheza mechi za kwanza, wapo ambao walicheza vizuri
na wengine kushindwa kuonesha viwango vyao.
Kwa wale
ambao walifeli katika mechiya kwanza,isiwe sababu ya kuwacheka na kuwakatisha tama
kwani ni mapema kupima viwango.
Bado kuna mechi
nyingi mbele ambazo zinatakiwa kuchezwa kwa kila timu. Kumbuka timu zipo 18 na kila
moja itacheza mechi 34.
Kucheza mechi
moja maana yake zimebaki 33, hivyo hapo mchezaji anaweza kubadilika na kuonesha
makali yake.
Wachezaji wengi
huwa wanafeli kuendana na hali ya ligi fulani hasa kwa wale wageni, hivyo ukiona
mchezaji kashindwa usimcheke, tazama namna anavyohangaika na utambue nini kimemfelisha.
Mifano ya wachezaji
wa aina hiyo ipo mingi, siyo Tanzania tu, bali dunia nzima. Utakuta mchezaji alipotoka
alikuwa tegemeo, lakini anapoenda ana kuwa hana msaada wowote.
Kupitia mechi
hizi za kwanza, tusipime viwango vya wachezaji, tuwape muda angalau mechi kumi,
kisha baada ya hapo ndiyo majibu ya kweli yatapatikana.
Yote kwa yote
tunataka kuona wachezaji wanapokuja kucheza soka Bongo walete ushindani wa kweli
nakuifanya ligi yetu kuwa miongoni mwa ligi bora Afrika.
Tuna
wachezaji kutoka mataifa mbalimbali kufikia 15 ambao kwa msimu huu wataonekana kwenye
LigiKuu Bara, hivyo kati ya hao, wapo ambao wataitangaza vema ligi yetu.
Mpaka sasa tunajivunia
uwepo wa Haruna Niyonzima, Meddie Kagere, Clatous Chama, Bernard Morrison na wengineo
ambao viwango vyao vimewafanya mashabiki wa soka hata waliopo njeya Tanzania
kuifuatilia ligi yetu.
0 COMMENTS:
Post a Comment