September 6, 2020

 


SVEN Vandenbroeck raia wa Ubelgiji ambaye ni Kocha Mkuu wa Simba, amewapa mchongo wachezaji wake wapya, Bernard Morrison na Larry Bwalya kwa kusema wana nafasi kubwa ya kuanza kikosi cha kwanza.

 

Kocha huyo ameweka wazi kwamba kila mchezaji ambaye yupo kikosini hapo anaweza kuanza katika kikosi cha kwanza endapo tu atapambania nafasi.

 

Mbelgiji huyo ameongeza kwamba, hakuna mchezaji ambaye ana nafasi ya moja kwa moja katika kikosi cha kwanza kwa sababu huu ni msimu mpya ambapo wamekuja wachezaji wengine wanaohitaji kuwatizama.


Kwa hapa licha ya kwamba kuna wachezaji wengi, kila mmoja ana nafasi ya kucheza na kuanza ndani ya kikosi cha kwanza.


“Hiyo inakuja kwa sababu huu ni msimu mpya na kuna wachezaji wengine tofauti na msimu ulioisha ambao ninahitaji kuwatazama, hivyo kwa yule ambaye atakuwa anapambania nafasi anaweza kucheza.

 

“Kitu kimoja ni kuwa nafurahia namna timu ambayo inaenda kwa sasa na naamini kama tutakuwa hivihivi hadi mwishoni mwa msimu tutakuwa tumefikia mafanikio makubwa,” alimaliza Sven.

 

Miongoni mwa wachezaji wapya ambao wametua Simba katika msimu huu ni pamoja na Bernard Morrison, Larry Bwalya, Chris Mugalu, Joash Onyango, Ibrahim Ame, Charles Ilanfya na David Kameta ‘Duchu.

1 COMMENTS:

  1. Msimu mpya wa ligi kuu TANZANIA bara unaanza kuna mengi ya kuzungumzia ligi hiyo.Mfano mimi siku shangaa kuona Harrison Mwakyembe akienguliwa ubunge kwani moja ya tatizo kubwa na lenye kutia aibu kwenye ligi yetu ni hali mbaya ya viwanja vya kuchezea mpira hasa ligi kuu.Tatizo la ubovu wa viwanja vyetu na kukosekana kwa viwanja bora kwa kiasi kibwa ndiko kunako dumaza mpira wetu na vilabu vyetu kukua. viwanja vyingi vya ligi kuu ndio chanzo cha umasikni wa vilabu vyetu vingi kwa kuwa ni vigumu kudhibiti mapato ya milangoni yasivuje kutokana na viwanja hivyo vingi vyao vinaweza kuruhusu matazamaji kuingia uwanjani kwa kupitia upande wowote ule wa uwanja wakipenda. Au hata shabiki akiamua kukaa nje ya uwanja basi ana uwezo wa kuona mechi bure. Mbaya zaidi viwanja vyingi vina sehemu ya kuchezea mpira zisiokuwa na viwango stahiki yaani pitch ni mbovu kabisa. Viwanja cha mpira kwa wenzetu ni mapambo vinamuhamasisha shabiki atake asitake aende uwanjani angalau akaone mandhari nzuri ya uwanja.Tunazungumzia CEO wa simba na Yanga lakini vipi CEO wa TFF ni nani na ana ubora gani wa kudadavua mambo ya kuboresha ligi zetu ili ziwe zinayojiendesha na ubunifu wa kuibua vipaji na ikiwezekana kuuzika nje ya nchi kwani watanzania wanapenda mpira teba sana, ni pesa hizo.Yaani ni pesa zinazotafuta mtu wa kuzikusanya laki wahusika wamelala usingizi fofo. Nani aliweza kuamini kuwa siku moja TANZANIA itajiendesha kwa kodi ya wananchi wake? Magufuli ameweza kwani taasisi nyengine zisiige miaka mitano imepita sasa tangu magufuli aje na mchaka mchaka wa kiutendaji ila kwa upande wa maboresho ya miundo mbinu ya viwanja vya mchezo ajira unaopendwa zaidi nchini yaani soka na unaoweza kwa kiasi kikubwa kuchangia pato la taifa bado halipewi uzito unaostahili. Umeskia waziri wetu wa utalii na kwa kiasi fulani ni kada wetu wa CCM ambayo ni mmiliki wa viwanja vyingi vya ligi kuu ambavyo havipo katika ubora stahiki ambae kwa dhamana yake ana nafasi kubwa ya kupambana kutumia utalii wa michezo kuitangaza nchi yetu lakini anaonekana kutumia nguvu kubwa mitandaoni kwenye kulunbana kwenye vitu vidogo. Kama TANZANIA tungekuwa na miundo mbinu bora ya viwanja vya soka tungethubutu kuandaa Afrika Cup. Kutokana na ubora wa kiigeographia wa nchi yetu ilipo ingelipa sana na kuitangaza nchi yetu kiutalii kimataifa na wakati huo huo kuinua hamasa ya michezo nchini.viwanja bora vya kuchezea mpira vinatengeza ligi bora na ndio maana south Africa na nchi nyengine za kiafrika zimetuacha mbali.viwanja bora vinatengeza matangazo bora na ya kuvutia kwenye tv yatakayohamasisha watazamaji wengi kuvutia wadhamini. Yaani ukweli usije ukaleta nongwa kwa wahusika lengo ni kujaribu kukumbushana jinsi gani tunazembea kufaidika na sekta ya michezo ambayo kwa kweli ni utajiri tunaouwacha upotee huku tukilia njaa. Tukiwa na viwanja bora hapana shaka hotel bora automatic zitakuwepo na kuboresha utalii hata wa ndani. Mambo ni mengi ya kufanya na kuleta faida kubwa kunako soka letu na kuzalisha ajira na ili watanzania kujitofautisha na wanaotuzunguka kabla ya wao kuja kuiwahi hii fursa tunatakiwa kubadilika na kwenda mwendo wa kasi kuboresha miundo mbinu yetu ya michezo ili kuitangaza nchi yetu na kuvutia watalii ni kama kutumia jiwe moja kupiga ndege wawili. Na hatuna haja kama nchi kwenda kujikweza kwa mataifa ya gharama kuboresha miundo mbinu yetu kwani tayari tuna urafiki mzuri wa kikazi na Uturuki. Waturuki wapo vizuri kwenye ujenzi wa miundo mbinu ya aina nyingi ni wajenzi mahiri.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic