September 6, 2020


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa hesabu zao kubwa kwa msimu mpya wa 2020/21 ni kuweza kutwaa kombe la Ligi Kuu Bara ambalo lipo mkononi mwa Simba.


Kauli hiyo ya uongozi wa Yanga ni ujumbe kwa Simba ambao nao leo wanaanza kurusha kete ya kwanza kwa kumenyana na Ihefu, Uwanja wa Sokoine majira ya saa 10:00 jioni.

 

Leo Yanga inatupa kete yake ya kwanza kwenye ligi kwa kumenyana na Tanzania Prisons Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku.

 

 Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa, uongozi wa klabu hiyo umejipanga kikamilifu msimu huu kuhakikisha wanafikia malengo waliyojiwekea ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ambao wameukosa kwa misimu mitatu mfululizo.


“Usajili tulioufanya msimu huu sio wa kitoto, umezingatia matakwa yote ya timu, wachezaji wapo katika kiwango kizuri tunachohitaji ni kuona tunafanikiwa kufanya vizuri kwenye ligi na kutwaa ubingwa mwisho wa msimu.

 

“Usajili ambao tumeufanya hatujaufanya katika kipindi cha misimu mitatu mfululizo, hivyo tunahitaji kufanya vizuri zaidi kwa kushirikiana na benchi la ufundi, wachezaji na uongozi kwa ujumla ili tupate matokeo mazuri,” amesema Mwakalebela.

 


6 COMMENTS:

  1. True! Vitendo uwanjani, kila mtu kasajili *mliosajili cyo wakina yipe kweli?* Ndoo ya nne mfululizo msimbazi hiyooo?*

    ReplyDelete
  2. Ni bora kwenda kimyakimya, kwani unapopata ushindi inakuwa mtamu sana kuliko kujipa tamaa ya kelele kwani mutapopigwa G4 tena itabidi mukimbilie fifa kuidai haki

    ReplyDelete
  3. WAZIRI KIGWANGALLA ASHANGAA MO DEWJI KUMTEUA MSAIDIZI WAKE BINAFSI KUWA CEO SIMBA
    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk HamisI Kigwangalla ametilia shaka uteuzi wa Msaidizi Binafasi wa Bilionea, Mohjamed ‘Mo’ Dewji, Barbara Gonzalez kuwa Mtendaji Mkuu mpya wa klabu ya Simba SC.
    Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, Mo Dewji leo amemtangaza Barbara Gonzalez kuwa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, akiziba nafasi ya Muafrika Kusini, Senzo Mazingisa Mbatha aliyehamia kwa watani, Yanga SC.
    Lakini saa chache baada ya uteuzi huo, Kigwangala akaandika kwenye ukurasa wake wa twitter; “Kuna ujanja na Kuna ujanja ujanja. Ujanja ni pale @SimbaSCTanzania tulipokubali kuhama kutoka kuwa Klabu ya Wanachama na kuwa Kampuni. Ujanja ujanja ni hiki kinachoendelea sasa hivi; hisa hazijalipiwa. PA wa mwekezaji ambaye hajalipia shares anateuliwa kuwa CEO,”.

    Kigwangalla ameongeza kwamba mabadiliko yaliyompa Mo Dewji Uenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC hayajakamilika kwa kuwa hajalipa Sh. Bilioni 20, lakini ajabu anafanya maamuzi anavyotaka.
    Mo Dewji akamjibu Kigwangalla katika mjadala uliovutia watu wengi wenye mawazo tofauti; “Mhe.Kigwangalla, sio utu kumuombea mtu yoyote apigwe mawe. Suala la uwekezaji Simba nililielezea kwenye interview na WasafiFM. Wengi wameelewa. Itafute. Kama bado hutaelewa, namba yangu unayo nipigie nitakufafanulia. Pia nisamehe kwamba mkopo wa pikipiki ulioniomba haikuwezekana,”.
    Hivi karibuni Mo Dewji alisema kwamba mfumo wa mabadiliko bado haujakamilika hivyo si wakati mwafaka kuzungumzia uwekezaji wake wa Sh. Bilioni 20 katika klabu hiyo. “Bilioni 20 zipo, kwa sasa kila mwaka natoa bilioni 3 kama ruzuku kwa klabu. Naamini asilimia kubwa ya Wanasimba wananielewa, kama hunielewi, basi,”alisema.

    ReplyDelete
  4. Kigwangala amekuwa akitumia account yake ya Twitter kuropokwa mambo nengi ya hovyo.Ni mtu mtu anaependa drama au sekeseke za kijinga. Kumbukwa alinusurika kutoka hatua cha chache tu kutumbuliwa na Magufuli kwa kutengeneza bifu nzito na katibu wake wizarani kiasi kwamba wakawa hawazungumzi.Sasa anamchokonoa Mo na inasemekana kisa kanyimwa mkopo wa piki piki za kampeni. Tulishasema zamani kingwala ajitafakari la sivyo uwaziri wake upo mashakani baraza jipya la mawaziri lijalo. Ni Mchapa kazi ila anapenda kujihusisha na drama za kijinga zisizomuhusu kama waziri mwenye zamana kubwa kwenye serikali ya tanz.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sawa lakn Umemshambulia tu hujajibu wasiwasi wake. Jibu anachojaribu kujiuliza.

      Delete
  5. Haina haja ya kujibu kwa sababu Moo amekwisha mjibu na alikwisha kujibu toka zamani kuwa kila kitu kinakwenda hatuahatuwa na aliyoyafanya pia ni zaidi ya hizo 20,000,000

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic