September 6, 2020

 


BERNARD Morrison, kiungo mpya wa Simba ambaye amesajiliwa kwa kandarasi ya miaka miwili rekodi zinaonyesha kuwa amewafunika nyota wote waliosajiliwa ndani ya Yanga ambao ni mabosi wake wa zamani.

Kwenye usajili uliofungwa Agosti 31, Yanga ilisajili wachezaji wapya 11 miongoni mwao ikiwa ni Tuisila Kisinda ambaye ni winga sambamba na Tonombe Mukoko kiungo mkabaji wote kutoka AS Vita ya Congo, Bakari Mwamnyeto beki kutoka Coastal Union na Michael Sarpong mshambuliaji kutoka Rayorn Sport ya Rwanda.



Simba wao walisajili wachezaji saba ikiwa ni pamoja na Morrison raia wa Ghana kutoka Yanga, Larry Bwalya kiungo kutoka Klabu ya Power Dynamo ya Zambia, Cris Mugalu mshambuliaji kutoka Lusaka Dynamo na Joash Onyango beki wa kati kutoka Klabu ya Gor Mahia ya Kenya.

Licha ya kwamba Simba imecheza mechi mbili za ushindani huku Yanga ikicheza mchezo mmoja wa ushindani, Morrison amekuwa wa moto kwenye mechi zote mbili mfululizo jambo ambalo linaonyesha kwamba akiendelea na moto huo atakuwa mfalme mpya ndani ya msimu wa 2020/21.

Alianza balaa lake Agosti 22 siku ya Simba Day wakati Simba ikishinda mabao 6-0 mbele ya Vital’O ya Burundi ambapo alihusika kwenye jumla ya mabao mawili kati ya manne, alifunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao.

Hakupoa kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii uliochezwa Agosti 30, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, wakati Simba ikishinda mabao 2-0 mbele ya Namungo alihusika kwenye mabao yote mawili ambapo alifunga bao moja na kusababisha penalti moja iliyofungwa na John Bocco.

 Morrison amehusika kwenye jumla ya mabao manne kati ya nane yaliyofungwa na amevaa medali ya kwanza akiwa Simba na kutwaa Ngao ya Jamii na kuwapoteza nyota wote wapya.

Wengine ambao wameanza kuonyesha makeke ndani ya Simba ni pamoja na Bwalya akiwa ametoa pasi moja ya bao kwenye mchezo dhidi ya Vital’O na Mugalu mwenye bao bao moja mbele ya Vital’O. Onyango ambaye ni beki ameonekana kuanza kufiti kikosi cha kwanza kwa kuwa imara kuokoa hatari ambapo hajashuhudia kipa wake akiokota mpira nyavuni.

Kwa upande wa wale wa Yanga, Sarpong ambaye ni ingizo jipya aliweza kuonyesha uwezo wake ndani ya uwanja ambapo alifunga bao moja kwa kichwa na Kisinda naye alipachika bao moja kwa guu lake la kulia.

Bakari Mwamnyeto ambaye ni ingizo jipya kutoka Coastal Union ameweza kuiweka ngome salama kwenye mchezo wake wa kwanza wa kirafiki wa kimataifa ambapo timu yake ilishinda mabao 2-0. Nyota mwingine ambaye ameanza kuonyesha uwezo wake ni Tonombe ambaye ni ingizo jipya kutoka AS Vita, pacha yake na Kisinda ikijibu inaweza kuwa balaa ndani ya msimu ujao.

5 COMMENTS:

  1. Simba ni mwalimu wa soka ambaye Kafanya mengi yakaigwa na wengine lakini waigaji hawajawahi kukiri na wala hawatokiri na wanapiga hufanya vile kama wao ndio walioanzisha Kati ya hayo ni Simba Day, kuwapamba suti wachezaji zinazopendeza, CO, kuleta wasanii kwa helicopta na mengineo lakini Mnyama hakuiga kitu, kwa mfano kuzungusha bakuli, kulalamika kwa kila kitu, kuzomea zomea, kuchana mashati na mengine

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ama kweli akili mali kuvaa suti na kupanda helicopta ndio mafanikio hayo asanter ndugu

      Delete
  2. Huwez kuweka mfananisho na watu ambao tayari wamezidi mechi. Utamfananishaj Morrison na TK master wakati unaona Morrison kazid mechi. Wacha kelele mwandishi, tulia Ligi ianze na halafu weka huo mfananisho wako

    ReplyDelete
  3. Hakuna timu hapo vyura aka kandambili mkishinda ni sare leo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic