September 2, 2020

 


KOCHA wa zamani wa Klabu ya Everton, Southampton na timu ya Taifa ya Uholanzi, Ronald Koeman kwa sasa amepewa mikoba ya kukinoa kikosi cha Barcelona.

Kocha huyo anachukua mikoba ya Quique Setien ambaye alitoka kupokea kichapo cha mabao 8-2 mbele ya Bayern Munich kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. 

Tayari ameshaanza maandalizi na timu hiyo kwa ajili ya msimu mpya wa La Liga, Agosti 31 na alianza bila ya uwepo wa staa wa timu hiyo, Lionel Messi ambaye yupo kwenye mvutano na mabosi wake akihitaji kusepa ndani ya kikosi hicho na timu inayotajwa sana ni Manchester City. 

Rekodi zinaonyesha kuwa Koeman alipokuwa ndani ya Klabu ya Everton alifukuzwa kutokana na matumizi makubwa ya fedha na kushindwa kuipa timu mafanikio.

Alifanya kazi na wachezaji wenye vipaji ikiwa ni pamoja na Sadio Mane,  Dusan Tadic na Graziano Pelle ndani ya Klabu ya Southampton ambao walichangia mafanikio yake ya kupata dili ndani ya Everton. 

Maisha yake ndani ya Everton yalikuwa magumu kwani mechi tisa zote za mwanzo alivurunda na kuifanya timu hiyo kuwa nafasi ya 18 na alipokea kichapo cha mabao 5-2 kutoka kwa Arsenal. 

Aliyeyusha jumla ya pauni milioni 140 lakini alifukuzwa baada ya miezi 16 ya kuajiriwa kutokana na kushindwa kuonyesha ubora ilikuwa ni mwaka 2016.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic