September 2, 2020


 IMEELEZWA kuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga raia wa Angola, Carlos St’enio Fernandez ‘Carlinhos’,  amekataa ofa ya kwenda kucheza soka la kulipwa Ureno na badala yake ameamua kuja kukipiga Jangwani.

 

Yanga chini ya wadhamini wao Kampuni ya GSM, hivi karibuni ilifanikisha usajili wa mshambuliaji huyo aliyekuwa anakipiga Interclube ya nchini Angola kwa ajili ya msimu ujao.

 

Kwa mujibu wa Injinia  Hersi Sai , ujio wa mshambuliaji huyo Yanga umewashtua watu wengi Angola, kwani walitarajia kumuona akienda kucheza soka Ureno.

 

“Ujio wa Carlinhos hapa Yanga umewashtua wadau wengi wa soka nchini Angola, kwani wengi walitarajia kumuona akienda kucheza soka Ulaya na siyo Yanga.

 

“Hiyo ni kutokana na kiwango kikubwa ambacho anacho hivi sasa kwani ni kati ya wachezaji nyota wanaotazamwa Angola.  Amekataa ofa ya kwenda kucheza soka la kulipwa Ureno,” alisema Hersi.


Nyota huyo kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi, Uwanja wa Mkapa alitumia dakika 9 uwanjani kuonyesha makeke yake kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Aigl Noir.


Yanga ilishinda kwa mabao 2-0 kwenye mchezo huo ambapo mabao yalifungwa na Michael Sarpon na Tuisila Kisinda.


Tamasha hilo lilikuwa na mvuto wa kipekee na lilipokelewa kwa utofauti na mashabiki wengi ambao walijitokeza uwanjani.


Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa kwa namna mashabiki walivyojitokeza wanastahili shukrani na kuwaomba waendelee kuipa sapoti timu yao bila kuchoka.

15 COMMENTS:

  1. Acheni sifa hakuna mchezaji anayeweza kugoma kwenda Ulaya aje Yanga ambayo haichezi mashindano ya kimataifa,ingekuwa kwenda club kubwa afrika kama tp mazembe tungesema sawa kwani kawa Ngasa?,acheni kusifia ujinga,tukutane October.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unapoandika uwe na kumbukumbu, mwaka jana tu Ibrahim Ajib alikataa kwenda TP Mazembe akazima simu, sasa anasugya benchi Simba, ambao wanapanga kumpeleka Namungo mwezi Desemba; kwenye dirisha dogo.
      Kupapatikia Ulaya ni kwa washamba, limbukeni wachache hasa ambao hawajafika, huyu mzazi wake mmoja ni mreno.

      Delete
    2. Labda ulaya ya Tandale.Hata Salehe Jembe akienda ulaya huaga anacheza mpira .

      Delete
    3. Mwaka jana John Bocco alichukua pesa za Orlando Pirates kisha akawazimia simu, kaibukia kuongeza mkataba Simba, sasa tunakaa naye Kinyerezi! Wabongo tunajijua wenyewe.

      Delete
  2. Tusidanganyene, hakuna mchezaji wa kukataa kwenda ulaya aje Tanzania. Kama ni kweli basi viwango vyake viko chini

    ReplyDelete
    Replies
    1. Faridi Mussa, Emmanuel Okwi, Shomari Kapombe na wengineo kwanini hawakukaa ulaya wakarudi kucheza hapa nyumbani?

      Delete
  3. Hatushangai ureno ndo utopolo, mpira anao alionao wa kwenda ureno. Kama Ni kweli kagoma back huyo shombeshombe Ni kiazi.

    ReplyDelete
  4. Sio ulaya tu,hata wa SPAIN NA WENGINE MAREKANI WAMESAIN YANGA,NYIE MIKIA FC VP?🤣🤣🤣🤣🤣🤣

    ReplyDelete
  5. YIPKE MDOGO WAKE DROGBA AU MSHASAHAU, TUSHAWAZOEA HAO WAZEE WA MPIRA WA MAGAZETINI NA REDIONI, WE ANGALIA KIPINDI HIKI MAGAZETI YANAUZA SANA KWA SABABU MASHABIKI WA HII TIMU WENGI MAMBUMBUMBU WAKIONA KITU KWENYE GAZETI WANAKICHUKUA KAMA KILIVYO HAWAPIMI

    ReplyDelete
  6. Ulaya ipi ya Morogoro.Kuna mjinga hapo anatoa mifano ya Okwi,Faridi na Kapombe. Wote hao walikwenda kucheza mpira na wakaishi huko.Na timu zwo zinajulikana.Tutajieni hiyo timu ya Ureno aliyeikataa?
    Au yale yale ya mdogo wake na Drogba??

    ReplyDelete
  7. Povuuu kungfu Kocha chali, hongera Kagere

    ReplyDelete
  8. Hao maboya hawakuongezewa mikataba wakarudi bongo,huyo anayetoa taarifa za Boko simba iko juu kwa viwango vya Fifa ukilinganisha na Orlando pyrates atoke simba?Ajibu alipokuwa Yanga magazeti ya bongo yalimkuza hakukuwa na Hilo dili,Magazet yanawadanganya utopolo,mchezaji yupi aliyetoka matopeni akaenda TP?acheni hizo.

    ReplyDelete
  9. ulaya ulaya hahahahaaaaa!wanatusahaulisha ya morrison hataree!huyo kakataa ulaya anajua hana kiwango cha kukipíga europe

    ReplyDelete
  10. Daraja la sita Ulaya ni sawa tu na kucheza Yanga.......atakuwa ana nia ya kucheza Simba kama kweli ni mzuri...anapita njia za ki Morrison.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic