September 30, 2020


 KIUNGO wa Yanga, Carlos Carlinhos raia wa Angola amepewa jukumu moja kubwa ndani ya kikosi hicho kwa kupiga mipira iliyokufa ikiwa ni kona pamoja na faulo.

Yanga ikiwa imefunga mabao manne ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 amehusika kwenye mabao mawili ambapo alitengeneza pasi za mwisho mbili ambazo zilileta mabao

 Mechi yake ya kwanza kuanza kipindi cha kwanza ilikuwa ni dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro wakati Yanga ikishinda bao 1-0.

Alitumia dakika 72 uwanjani na dakika ya 61 kwenye mzunguko wa nne alitoa pasi ya bao ya pili kwa Lamine Moro na kumfanya awe kinara wa pasi za mwisho ndani ya Yanga akiwa nazo mbili.  

Pasi yake ya kwanza aliitoa Uwanja wa Mkapa wakati Yanga ikishinda bao 1-0 mbele ya Mbeya City ambapo pia alipiga kona iliyokutana na Lamine aliyepachika bao lake la kwanza kwa kichwa. Yanga kwa sasa inajiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 3, Uwanja wa Mkapa.


Leo itakuwa na kibarua cha kumenyana na KMKM ya Zanzibar kwenye mchezo wa kirafiki utakaopigwa majira ya saa 1:00 usiku Uwanja wa Azam Complex.


Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema kuwa nyota huyo anakipaji na uwezo ambao unafanya akiwa ndani ya uwanja asumbuliwe.


"Carlinhos ni mchezaji mzuri na akiwa ndani ya uwanja amekuwa akipata usumbufu mkubwa imani yetu ni kwamba atakuwa bora zaidi akizoea," 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic