September 9, 2020



NYOTA wa timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo anakuwa mchezaji wa pili kwa wachezaji wa mpira wa miguu duniani kufunga mabao 100 kwenye timu yake ya Taifa baada ya kufanya hivyo usiku wa kuamkia leo wakati timu yake ikimenyana na Sweden kwenye mashindano ya Nations League.

Wakati Ureno ikishinda kwa mabao 2-0, mabao yote yalifungwa na nyota huyo ambapo alianza kufunga bao la kwanza dakika ya 45 na lile la pili alipachika dakika ya 72 na wapinzani wao Sweden walimaliza wakiwa pungufu baada ya nyota wao Gustavv Svensson kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 44.

Anakuwa nyota wa kwanza wa Ulaya kuifikia rekodi ya nyota wa Iran, Legend Ali Daei ambaye alifunga jumla ya mabao 109 huku yeye akiwa na mabao 101.

 Ronaldo amekuwa kwenye ubora wake ndani ya uwanja akiwa na ushkaji mkubwa na nyavu na msimu ulipita aliweza kufikisha jumla ya mabao 700 kwenye mashindano yote ndani ya uwanja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic