September 9, 2020

 


ZLATKO Krmpotick, Kocha Mkuu wa Yanga raia wa Serbia ana kibarua kizito cha kumalizana na vigingi vitatu ndani ya dakika 270 kwenye mechi zake za mwezi Septemba zilizo karibu kwa sasa ndani ya Ligi Kuu Bara.

Mchezo wake wa kwanza kukaa benchi baada ya kupokea mikoba ya Luc Eymael ilikuwa ni Septemba 6 Uwanja wa Mkapa alishuhudia balaa la Wajelajela, Tazania Prisons, wakiwapigisha gwaride wachezaji wake kwenye sare ya kufungana bao 1-1.

Kigingi chake kinachofuata ni dhidi ya Mbeya City, Septemba 13, Uwanja wa Mkapa.Ana kazi ya kuweka rekodi mpya kuziokoa pointi sita mbele ya Mbeya City kwa kuwa msimu uliopita Yanga iliambulia pointi mbili na kuyeyusha pointi nne.

Mchezo wa kwanza msimu uliopita ambao uliwakutanisha Mbeya City na Yanga, Uwanja wa Sokoine ziligawana pointi mojamoja kwa sare ya bila kufungana na walipokutana mara ya pili Uwanja wa Mkapa, ngoma ilikuwa ni 1-1.

Kigingi cha pili ni Kagera Sugar na mchezo huu utapigwa nje ya Dar ukiwa ni mchezo wa kwanza kwake mkoani na itakuwa ni Septemba 19, Uwanja wa Kaitaba.

Msimu uliopita walipokutana Uwanja wa Uhuru, Kagera Sugar iliwagonga nyingi Yanga kwa kuwatungua mabao 3-0 na mchezo wa pili uliochezwa Kaitaba, Yanga ilishinda bao 1-0.Hivyo kwenye pointi sita waligawana pointi tatutatu.

Ataiaga Septemba kwa kumalizana na kigingi cha pili ambao ni Mtibwa Sugar itakuwa pale Uwanja wa Jamhuri, Septemba 27.

Mchezo wa kwanza msimu uliopita walipokutana Uwanja wa Mkapa, Yanga ilishinda bao 1-0 ule wa pili uliochezwa Uwanja wa Jamhuri ngoma ilikuwa 1-1. Yanga ilisepa na pointi nne na kuyeyusha mbili kati ya sita hivyo kazi itakuwa nzito msimu huu.

3 COMMENTS:

  1. binadamu tunapishana kufikria..ukilinganisha na pale Mbeya City ilipoishia na msimu uliopita na pale imeanzia msimu huu...pia ukifikiria kikosi cha bilioni 1.5 cha Yanga huo mchezo kati ya Mbeya sio kizingiti hata kidogo..Tunajua huko baada ya matokeo Prison kocha kaomba muda ili asuke timu..ila vizingiti vya ukweli tunavijua

    ReplyDelete
  2. Unatoka Kagera unarudi Morogoro, ni mateso sana haya

    ReplyDelete
  3. mbona Simba katoka Mbeya anarudi tena Morogoro?
    Utopolo wao waache wainjoy kuchezea mechi mbili mfululizo za kufungua nyumbani..ingekuwa ni Simba na Zahera kaanza mbili ugenini hapo angekuwa ameishaliamusha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic