September 4, 2020


 KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji Sven Vandenbroeck amefunguka kwamba straika wake, Meddie Kagere anakaa benchi kutokana na yeye kupanga na kuchagua timu kutokana na aina ya timu ambayo anaenda kukutana nayo kwenye mechi zao.

 

Kocha huyo ameongeza kwamba pia amekuwa akiangalia zaidi mafanikio ya timu yake katika kushinda na wala siyo mtu mmoja huku kila mchezaji aliye hapo anaweza kukaa benchi kutokana na atakavyokuwa anawaona wapinzani wake.

 

Kagere ambaye alikuwa mfungaji bora wa timu hiyo kwa msimu uliopita, amekuwa akikosa nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo ikiwemo katika mechi ya Ngao ya Jamii mbele ya Namungo FC ambapo Simba walishinda mabao 2-0.


Sven amesema kwamba hakuna tatizo la Kagere kukaa benchi ndani ya timu hiyo kutokana na hali hiyo inaweza kumkuta mchezaji yeyote ndani ya kikosi hicho kwa sababu ya kuangalia mafanikio zaidi ya kikosi hicho kuliko mtu binafsi.


“Kuhusiana na Kagere wala hakuna tatizo lolote lile la yeye kukaa benchi kwa sababu hilo linaweza kumtokea kila mchezaji aliye hapa.

 

“Nachagua timu kutokana na mfumo ulivyo na namna tunavyocheza, sijui kwa nini watu wanazungumzia kuhusiana na mtu mmoja.

 

“Naangalia mafanikio zaidi ya timu, kama tunashinda iwe timu na hata tukipoteza ni kwa ajili ya timu na hata tuchukue mataji ni timu, siyo mtu mmoja.


“Lakini vilevile anaweza kutumika kwenye mechi zetu zinazokuja mbele na wengine wakakaa tu nje,” alimaliza Mbelgiji huyo.

10 COMMENTS:

  1. Huyu kocha kiazi mfungaji bora miaka miwili mfululixo unamweka benchi unampa nafasi boko huku mechi kibao anakosa magoli ya wazi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bocco ana msaada sana kwenye team kuliko Kagere, si mbinafsi, anatengenezea wenzake nafasi za kufunga kitu ambacho kwa MK14 ni nadra always anataka afunge yeye hata akiwa angle ngumu

      Delete
  2. Sasa simnasajili wazee, ndio maana ngumi ziliwaka

    ReplyDelete
  3. Harufuya ugomvi huu ilianza zamani,hata kama hawajapigana lakini inaonekana kabisa kwamba kuna jambo linafukuta. Huyu kocha aliwahi kuwafukuza waandishi kama mbwa wakati wa mazoezi ya team yao ikijiandaa na mchezo wa FA, hadi kapteni Boko aliingilia kati n alitoa maneno ya kashfa sana, kama sio hekima za TFF wangemlipua sana. Nadhani moshi huu ukiachwa kuna siku utawasha moto, nasikitika zaidi kwamba makocha wa kigeni wanatudharau, kama ilivyokuwa yule mpuzi lucy wa Yanga, nilitamani kabla hajaondoka awekwe ndani maana huo ubaguzi na dharau wanazotufanyia tena nchini kwetu ni mbaya sana. Ukiwa kwao huwezikuthubutu kufurukuta. Lazima tufanye kitu.

    ReplyDelete
  4. Issue ya makocha wa soka ni ulimwenguni kote.Makocha wanaweza waka kujenga na kuwa mchezaji bora na wanaweza waka-kubomoa ukawa ovyo na mchezaji akapotea.Mifano iko mingi sana na tusiende mbali na tuangalie yaliyo wahi kuwakuta baadhi ya wachezaji nchini Tanzania.Hamisi Tambwe akiwa Simba chini ya kocha Patrick Phiri hakuwa akimpa nafasi ya kucheza kwa madai mchezaji huyo hakuwa anakaba zaidi ya kuwa mviziaji hivyo akapotezewa na Hans Puljim akijiokotea embe dodo chini ya mbuyu akamkaribisha Yanga na hii ilisababisha Patrick Phiri kufungiwa virago.Yusuf Mpilipili alikuwa mmoja wa defenders aliyeaminiwa na makocha Omog na baadaye Lenchatre na hata Masoud Djumaa lkn Simba ilivyokuwa chini ya Aussems na sasa Sven then Yusuf Mpilipili akasugua benchi.Kaseja enzi za Maximo tulimsahau kama mmojawapo wa makipa bora mwenye kipaji kutokea Tanzania lkn alikuwa anapigwa benchi ktk timu ya Taifa bila ya sababu.Jonas Mkude amanusura naye apotee kwa kuwekwa benchi wakati wa kocha Omog lkn alivyoingia kocha Lenchatre akarudi ktk ubora wake.Rashid Juma chini ya Omog na Aussems alikuwa anapewa nafasi hadi alicheza dhidi ya AS Vita na alikiwasha kweli lkn alivyokuja Sven sikumbuki ni mechi gani alichezeshwa.Na haya yamewakuta wachezaji wengi kama Ally Mtoni na kocha Luc, Ajib, Kagere na kocha Sven.Kwa maisha ya mchezaji kama anataka asipotee ktk dimba la soka ni muhimu wao kuondoka bila ya kusubiria mkataba uishe na ikiwezekana ni kuvunja mkataba na kwenda kujaribu maisha ya soka ktk klabu nyingine na huwezi kujua kwani ni Mwenyezi Mungu ndio anayepanga kuliko kung'ang'ania sehemu wakati kocha hana mipango na wewe kwani wakati ni ukuta.

    ReplyDelete
  5. Kwahiyo mwenye blog uzalendo umekushimda?

    ReplyDelete
  6. kocha awez kuchezesha wachezaji mnayemtaka nyie atachezesha timu ya ushindi ndo wabongo unalazimisha mlipili acheze wakat kuna wachezaji bora zaidi yake pale simba hawaangalii majina ni kiwango

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic