September 30, 2020


 ZIKIWA zimebaki siku 17 kwa Yanga na Simba kukutana Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, rekodi zinaonyesha kuwa ndani ya dakika 180, Simba imewapoteza  Yanga kwenye mechi zao ambazo wamecheza Uwanja wa Mkapa kwa kufunga mabao mengi.

Yanga ambao ni wenyeji wa mchezo huo wameutumia Uwanja wa Mkapa kwenye mechi mbili za ligi, ambapo walianza mchezo wa kwanza mbele ya Tanzania Prisons ambapo ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na mchezo wa pili uliokamilisha dakika 180 ilikuwa ni mbele ya Mbeya City wakati Yanga ikishinda bao 1-0.

Ikiwa imecheza mechi mbili Uwanja wa Mkapa, Yanga imefunga mabao mawili na kuruhusu kufungwa bao moja ikipotezwa na Simba ambayo imecheza mechi mbili Uwanja wa Mkapa na kufunga jumla ya mabao saba na nyavu za Aishi Manula hazijatikiswa.

Mechi ya kwanza ya Simba, Uwanja wa Mkapa ilikuwa dhidi ya Biashara United wakati ikishinda mabao 4-0 kisha ilishinda mabao 3-0 mbele ya Gwambina FC na kuifanya iwe inaidai Yanga mabao matano kwa mechi zao walizocheza Uwanja wa Mkapa.

Mabao ya Yanga Uwanja wa Mkapa yamefungwa na nyota wawili wakigeni ambao ni Michael Sarpong ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons na Lamine Moro mbele ya Mbeya City huku yale ya Simba yakifungwa na Clatous Chama aliyepachika mawili, Meddie Kagere mawili na Chris Mugalu mawili na Pascal Wawa bao moja.

3 COMMENTS:

  1. Huo ni upuuzi tena uliovaa chupi, yani unataka kuniambia et mechi 4 ndo tuanze kufikilia mfungaji bora! Acheni uzwazwa

    ReplyDelete
  2. YANGA YAIPOTEZA MAZIMAMAZIMA SIMBA KWENYE MECHI ZA UGENINI.

    Wafalme wa soka la bongo Yanga, kwa msimu huu wamewapoteza mahasimu wao wa kubwa Simba, kwa kuvuna alama nyingi za UGENINI, ikiwa Yanga wamepata point 6na huku Simba wakiambulia point 4.......HATA SISI TUNAWEZA KUANDIKA HIVYO

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic