September 2, 2020

 


SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa hana tatizo na nyota namba moja wa kucheza na nyavu ndani ya Simba Meddie Kagere.

Habari zinaeleza kuwa wawili hao walipigana jana baada ya kutofautiana jambo ambalo lilisambaa kwenye mitandao ya kijamii huku uongozi wa Simba ukikanusha kwamba hakuna ukweli katika hilo.

Sven amesema kuwa:- "Siwezi kutumia nguvu kwenye mambo yasiyo ya maana ambayo sijui yanatoka wapi. Mimi sina tatizo, Medie hana tatizo hilo ndilo ninaweza kusema."

Kagere ndani ya Bongo kwa misimu miwili mfululizo amesepa na tuzo ya mfungaji bora ambapo msimu wa 2018/19 ikiwa ni msimu wake wa kwanza alitupia mabao 23.

Msimu wa 2019/20 alitupia mabao 22 na kufanya afikishe jumla ya mabao 45 ndani ya Ligi Kuu Bara.

Kwa sasa Simba imeanza maandalizi ya mchezo wao wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Septemba 6, Uwanja wa Sokoine, Mbeya dhidi ya Ihefu.

10 COMMENTS:

  1. Basi mrudishie power bank yake

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tunataka tukachukue nyingine hii sasa hv naona imesha expire ili aendelee kuwa mfungaji bora na tarehe 18 ziwe 5G na sio 4G SHENZIIII NIMEKUKERAAAAAA EEH

      Delete
  2. Kagere fanya yko hata dk 10 tu ukipewa tupia mabao Kama yote, utopolo wafunge domo

    ReplyDelete
  3. Lkn ukiangalia vizuri picha Kocha ana uvimbe shavuni karibu na kisogo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Simba inakeraaaaaaaaaaaaaaaa!, hata mimi nimekuona ulikuwa unaandika huku machozi yanakulenga poleeee, tunawakeraaaaaaaaaaa

      Delete
  4. Kagereeee piga kama MWAKINYO mpaka wakuruhusu kuondoka maana wana kukomalia kwa mambo ya kipuuzi, kwahiyo next time pasua na manara arafu vunja mkataba.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Eeh nyani anaota, anafikiri yupo kwenye shamba la mahindi teh teh teh teh, tunawakeraaaaaaaaaaaa tu mpaka mjinyonge shenziii,habari zilizotufikia hivi punde Simba wanaomba radhi kwa kutoa kipigo finyu cha goli 4-1 kwa chura f.c

      Delete
  5. Acheni ujinga na wivu misimu 2 mfululizo yeye ndio mfungaji bora na huu wa 3 napo atakuwa mfungaji bora

    ReplyDelete
  6. Piganeni tu. kwani mukipigana Siyo ajabu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic