September 30, 2020


 KIKOSI cha Yanga leo Septemba 30 kimeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya KMKM kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Tonombe Mukoko dakika 10 kwa kona ya Carols Carinhos kiungo ambaye amepewa jukumu la kupiga mipira iliyokufa ndani ya Yanga.


Dakika 20 mbele Mukoko tena alipachika bao la pili na la mwisho wa timu yake baada ya mabeki wa KMKM ya Zanzibar kujichanganya katika harakati za kuokoa hatari.


Kipindi cha pili mambo yalikuwa magumu kwa KMKM kuweza kuweka mzani sawa huku Yanga nao pia wakikwama kuongeza bao la pili. 

Mchezo wa leo ulikuwa ni wa kirafiki ambapo lengo kubwa ni kukiweka kikosi sawa cha Yanga fiti kwa kuwa hakikuwa na mazoezi ya muda mrefu kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2020/21 kutokana na janga la Virusi vya Corona kutibua ratiba nyingi duniani. 

Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema kuwa malengo makubwa ni kukiandaa kikosi kwa ajili ya mechi zao zinazofuata.


"Kikosi kilikuwa na muda mfupi kwa ajili ya maandalizi ya ligi hivyo kwa sasa tunazidi kujiimarisha ili kuwa bora hasa ukizingatia kwamba tuna wachezaji wengi wapya," amesema.

9 COMMENTS:

  1. Kwa Namna nilivowaona KMKM, ingelikua Mnyama wangeondoka na si chini ya mabao sita

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani Mnayama ndio nini? Mbona alishindwa kumfunga Mtibwa na sisi tukamfunga?

      Delete
    2. Kwani mmeomba kucheza nao wakagoma?

      Delete
  2. Waambie wacheze nao mbona wapo tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bado mapema tulia mwananchi acha kupigizana kelele na majukwaa.

      Delete
  3. Kwani haukuona kama na mtibwa mlikuwa kichawi zaidi? Timu ya utopolo ni mbovu, asipocheza mukoko na kisinda hamshindi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tatizo hamjui kuwa mikia inabebwa na nan mpaka mnahesabu kosa mtu fulan hawashindi.Ndio maana ya usajili bhana usipayuke bila sababu

      Delete
    2. Kwani ni wachezaji wa timu gani hadi wasiruhusiwe kuichezea Yanga. Au ulifikiri wameletwa Tanzania kuja kutalii???

      Delete
  4. Kumaliza ubishi Utopolo waombe friend match na Mnyama wikiendi hii

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic