September 28, 2020


 JUMA Mwambusi, Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa kwa namna kikosi ambavyo kinatengenezwa kwa sasa kuna timu itapigwa mabao 10 ndani ya dakika 90.


Yanga jana Septemba 27 iliibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.


Bao pekee la ushindi lilifungwa na beki kisiki wa Yanga, Lamine Moro dakika ya 61 akimalizia mpira wa pigo la kona lililopigwa na Carlos Carinhos.


Mwambusi amesema:"Tunazidi kukijenga kikosi kwa sasa na kwa namna ambavyo tunakuja hivi kuna timu itafungwa mabao 10,8 na kuendelea.


"Kikubwa ambacho tunakihitaji ndani ya uwanja ni pointi tatu hivyo kwa sasa mashabiki waendelee kutupa sapoti mambo mazuri yanakuja." amesema.


Yanga ipo nafasi ya tatu ina pointi 10 kibindoni baada ya kucheza mechi nne sawa na watani zao wa jadi Simba ambao wapo nafasi ya pili wakitofautiana kwenye idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.


Simba imefunga mabao 10 na Yanga imefunga mabao manne ndani ya ligi kwa msimu wa 2020/21.Kinara ni Azam FC ambaye hajapoteza mchezo hata mmoja kati ya minne akiwa na pointi 12 na mabao matano kibindoni.

8 COMMENTS:

  1. Mnawaza goli kumi wakati hamna hata mechi moja mmeshinda zaidi ya goli moja yaqle maneno ya Eymael yanawahusu zaidi ya washabiki

    ReplyDelete
    Replies
    1. inaonekana ubongo wako hauna uwezo mzuri wa kuelewa ndugu yangu,uelewa wako ni mdogo.....amesema kwa jinsi ambavyo kikosi kinatengenezwa kuna timu itapigwa kumi.kwa mtu muelewa nadhani amemwelewa kuwa kwa sasa timu bado haijawa tayari ki muunganiko ndio maana inashinda goli chache,lakini itakapokuwa tayari hayo ndio yanaweza kuwa matokeo.

      Delete
    2. Nyie si mmecheza na timu zilizopanda aka vibonde

      Delete
    3. yani unmwambia mwenzio ubongo wako hauna uelewa mzuri mara uelewa wako mdogo mi nafikiri wewe unayemuona mwenzio uelewa wake mdogo wewe ndio utakuwa una uelewa mdogo zaidi ya huyo uliyemkosoa kama unashindwa kuchekecha ubongo wango kwa kila neno linalotamkwa na kocha wenu

      Delete
    4. Nyie si ndio kocha aliwaambia uneducated mnazungumziaje goli kumi wakati ushindi wenu hamjawahi kuzidisha zaidi ya goli mbili halafu unajiona ubongo wako umefanya kazi Eymael hakukosea

      Delete
  2. Huu sasa usanii, unafikiria kupiga goli kumi wakati unafunga goli mojamoja yena la mipira ya kutenga. Hadi unamaliza kusuka kikosi ligi itakuwa imeisha.

    ReplyDelete
  3. Hana jipya Huyo ni kujitetea tu mashabiki wasiojielewa watamkubali,tim haina muunganiko wowote kila mtu anacheza kivyake.

    ReplyDelete
  4. Labda mpate faulo 20 ndio mtafunga 10 maana refa wa Jana hovyo kweli kawanyima penalty mtibwa halafu wao magori yenyewe ya kona na faulo hakuna gori la move strike wamelala Sasa akibanwa lamine Kuna kazi hapo mi nawaambia yanga ya mwaka huu ndio mbovu kabisa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic