ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa makosa ambayo wameyafanya kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga watayafanyia kazi ili kuweza kurejea kwenye ubora ambao walianza nao.
Mtibwa Sugar, ilipoteza mchezo wake wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara jana Septemba 27 kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Yanga mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Kabla ya mchezo wa jana, Mtibwa Sugar ilicheza mechi tatu ambazo ni dakika 270 na haikupoteza kwa kuwa ililazimisha sare ya bila kufungana na Ruvu Shooting Uwanja wa Gairo kisha ikalazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Simba Uwanja wa Jamhuri na imeshinda mchezo mmoja kwa kushinda bao 1-0 mbele ya Ihefu FC Uwanja wa Sokoine.
Katwila amesema kuwa :"Ni makosa madogo ambayo tumeyafanya na nimeyaona hivyo ninachokifanya kwa sasa ni kuweza kufanya marekebisho na kutazama namna gani tutakuwa imara.
"Ushindani ulikuwa mkubwa na kila mchezaji aliweza kujitahidi kwa nafasi yake kusaka matokeo ila mwisho wa siku mambo yamekuwa namna hiyo tumepoteza pointi tatu hatujapoteza matumaini.
"Kuna mechi za kucheza nyingine zipo mbele yetu huko hivyo tunajipanga vizuri kupata matokeo mazuri."
0 COMMENTS:
Post a Comment