October 7, 2020


 KOCHA wa viungo wa Klabu ya Yanga, Riedoh Berdien amefunguka kuwa ni suala la tiketi tu ndiyo ambalo linaendelea kumkwamisha kurejea nchini kujiunga na kikosi cha timu hiyo kwa kuwa tayari amekamilisha muda wake wa mapumziko aliokuwa amepewa na uongozi wake.

 

Kutokana na ruhusa hiyo, Berdien amekosekana kwenye michezo mitatu iliyopita ambapo Yanga ilishinda kwa kuzifunga Mbeya City, Kagera Sugar, Mtibwa Sugar na Coastal Union.

 

 Berdien amesema kwa sasa amekamilisha kushughulikia dharula aliyokuwa nayo na kila kitu kimekaa sawa.

 

“Tayari nimekamilisha muda wangu wa likizo ya dharula niliyokuwa nimepewa na uongozi ambapo nilirejea nyumbani Afrika Kusini, hivyo nimewasiliana na uongozi kwa ajili ya taratibu za kushughulikia suala la kunitumia tiketi ili niweze kurejea kazini.

 

“Unajua kwa sasa hivi Afrika Kusini ipo katika daraja la kwanza ‘level one’ ya usitisho wa shughuli mbalimbali ‘lock down’ kutokana na janga la Virusi vya Corona lakini ndege zinaruhusiwa kuingia na kutoka, inawezekana nikarejea,” amesema Berdien.

 

Yanga ipo katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara na pointi zao 13 baada ya kucheza mechi tano.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic