October 15, 2020


 KOCHA Cedric Kaze anayekuja kushika mikoba ya kuifundisha Yanga, yupo safarini kuja nchini Tanzania kwa ajili ya kuanza rasmi majukumu yake mapya.


Ofisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli, amethibitisha ujio wa Kocha huyo ambaye mapema leo alikuwa jijini Amsterdam Uholanzi, kwaajili ya kubadilisha ndege ya kumleta Tanzania.

Kaze anatarajiwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere majira ya saa nne usiku leo kwa ndege ya Shirika la Ndege la KLM.

Anakuja kubeba mikoba ya Zlatko Krmpotic ambaye alifungashiwa virago Oktoba 3 baada ya kumaliza mchezo dhidi ya Coastal Union.

Wakati anaondoka aliacha timu ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 13 kisha ilishushwa na Azam FC baada ya kushinda dhidi ya Kagera Sugar na Simba iliposhinda mabao 4-0 dhidi ya JKT Tanzania ikashushwa mpaka nafasi ya tatu.

3 COMMENTS:

  1. Mwambieni aje na begi lake moja dogo tu la nguo na vitu muhimu maana akae huku akijua anakuja Jangwani Big Brother house

    ReplyDelete
  2. Asubiri nae afukuzwe tarehe 7 baada ya mechi tumechoka na hadisi za huyo kocha kocha

    ReplyDelete
  3. Hakuna cha kuandika tumechoka na kocha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic