October 15, 2020


 PAUL Pogba ametoa kauli ambayo inamaanisha au inaonyesha kuwa anaweza kuondoka ndani ya Manchester United, hiyo ni baada ya kusema kuwa anatamani kuichezea Real Madrid.

 

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27, mkataba wake unatarajiwa kumalizika miezi 10 ijayo, na hadi sasa hakuna mazungumzo ya mkataba mpya kuhusu kuendelea kuichezea timu yake hiyo.


Uongozi wa United chini ya Mtendaji, Ed Woodward haujazungumza chochote na staa huyo licha ya kuwa muda wa mkataba wake unaelekea ukingoni.

 

Pogba aliwahi kuhusishwa kuondoka klabuni hapo lakini ukimya ulitawala hasa baada ya kuingia kwa maambukizi ya Virusi vya Corona, ambapo wakala wake, Mino Raiola alikuwa akiituhumu United wakati huo kuwa haina mwelekeo.


Licha ya kuwa bado ni mchezaji wa kikosi cha kwanza, Pogba amesema: “Kila mchezaji anapenda kuichezea Real Madrid.Ni ndoto kwangu, kwa nini nisiichezee?


“Nipo Manchester na ninaipenda klabu yangu, ni mchezaji wa Manchester, ninafurahia uwepo wangu hapa.Nitaendelea kucheza kwa nguvu zote na kusaidiana na wenzangu.”


Manchester United kwa sasa ipo katika kipindi kigumu hasa baada ya kufungwa mabao 6-1 dhidi ya Tottenham Hotspur, wiki iliyopita.


Mbali na hapo United imemkosa Jadon Sancho katika dirisha la usajili lililofungwa wiki iliyopita.

Hivyo, kutokana  Pogba ametoa kauli ambayo inamaanisha au inaonyesha kuwa anaweza kuondoka ndani ya Manchester United, hiyo ni baada ya kusema kuwa anatamani PARIS, Ufaransana kauli hiyo ya Pogba inamaanisha kuwa United sasa inaingia katika sakata jipya la mkataba la Mfaransa huyo, kama imuache abaki hadi mwisho wa msimu aondoke bure au impe mkataba mpya.


Pogba aliongeza: “Sijazungumza na yeyote, sijazungumza na Ed Woodward. Hatujazungumza kuhusu dili jipya, kwa sasa nipo Manchester na akili yangu ni kupambana kurejea kuwa kwenye kiwango kizuri.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic