October 19, 2020


 

KITENDO cha Kocha Mkuu wa Geita Gold ya Geita, Fred Felix Minziro kuiwezesha timu hiyo kushinda michezo miwili katika Ligi Daraja la Kwanza kimevunja rekodi ya timu hiyo ya misimu minne ambapo walishindwa kufabnya hivyo kwenye mechi hizo wakiwa nyumbani.

 

 

Minziro kwa sasa ana kibarua cha kusaka tiketi ya kuipandisha Geita Gold baada ya kuweza kufanya hivyo alivyokuwa ndani yaSingida United na KMC kwa nyakati tofauti.


Aliibuka ndani ya Geita Gold baada ya kukwama kuibakisha ndani ya ligi Klabu ya Mbao FC ambayo inapambana nayo Ligi Daraja la Kwanza huku ikiwa na mwendo wa kusuasua kutukana na kusumbuliwa na tatizo la ukata. 

Minziro amesema: “Nashukuru sana Mungu kwa kupata matokeo kwenye michezo miwili, hali hii imetupatia kujiamini na sasa akili zetu tunazielekeza katika mchezo ujao dhidi ya Alliance ya Mwanza kwa kuwa malengo yetu ni kupata pointi za mapema zitakazotuwezesha kupanda daraja mapema iwezekanavyo.”

 

 Geita Gold imeanza vizuri ndani ya Ligi Daraja la Kwanza na ina kumbukumbu ya kuishia hatua ya play off msimu uliopita iliposhindwa kupenya mbele ya Mbeya City inayonolewa na Kocha Mkuu, Amri Said.


Pia hata msimu wa 2018/19 iliishia hatua hiyo baada ya mbio zake kugonga mwamba mbele ya Mwadui FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic