October 19, 2020

 


SALUM Kihimbwa nyota wa Mtibwa Sugar FC leo Oktoba 19 amefunga bao lake la kwanza ndani ya msimu wa 2020/21 wakati timu yake ikishinda bao 1-0 dhidi ya Namungo FC. 

Mchezo wa leo umechezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ukiwa ni wa kwanza kwa Mtibwa Sugar kucheza ikiwa chini ya kocha msaidizi, Vincent Barnaba baada ya Zuber Katwila aliyekuwa Kocha Mkuu,  kubwaga manyanga jana, Oktoba 18.


Kwa sasa Katwila yupo na Ihefu FC ambapo alitangazwa jana Oktoba 18 kuwa Kocha Mkuu ndani ya kikosi hicho chenye maskani yake Mbaye ambacho kesho kitashuka Uwanja wa Sokoine kumenyana na Azam FC.


Kihimbwa alipachika bao lake hilo kwa mkwaju wa penalti na kuifanya Mtibwa Sugar kusepa na pointi tatu mazima mbele ya Namungo FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Hitimana Thiery.


Ushindi huo unaifanya Mtibwa Sugar kuwa nafasi ya 12 kwenye msimamo ikifikisha jumla ya pointi nane baada ya kucheza mechi saba huku Namungo FC ikiwa nafasi ya nane baada ya kucheza mechi saba na ina pointi nane ikiizidi Mtibwa Sugar idadi ya mabao ya kufunga.


Namungo imefunga jumla ya mabao manne huku Mtibwa Sugar ikiwa imefunga mabao matatu ndani ya ligi kwa msimu huu wa 2020/21.


Kinara ni Azam FC mwenye pointi 18 akiwa amecheza mechi sita na zote ameshinda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic