MWINYI Zahera, Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi ndani ya Klabubya Gwambina FC, leo Oktoba 19 alikuwa ndani ya Uwanja wa Sheik Amri Abeid akishuhudia timu yake ikigawana pointi mojamoja na Klabu ya Polisi Tanzania baada ya sare ya kufungana bao 1-1.
Stive Jimmyson alipachika bao kwa upande wa Gwambina FC huku lile la Polisi Tanzania likipachikwa na Hamad Ally na kuwafanya wagawane pointi mojamoja leo kati ya zile tatu walizokuwa wakizisaka.
Ushindi huo unaifanya Polisi Tanzania kuwa nafasi ya tano ikiwa na pointi 11 baada ya kucheza mechi sita huku Gwambina FC ikifikisha jumla ya pointi nane ikiwa nafasi 9 kwenye msimamo.
Safu ya Gwambina FC Kwenye mechi saba ilizocheza imefunga mabao matano huku Polisi Tanzania ikiwa imefunga mabao saba Kwenye mech zao sita.
0 COMMENTS:
Post a Comment