CHRIS Mugalu mshambuliaji namba mbili ndani ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck amesema kuwa anataka kufunga zaidi ya mabao 15 kwenye Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21.
Mshambuliaji
namba moja kwa sasa ni Meddie Kagere ambaye kwenye ligi amefunga mabao manne
akifuatiwa na Mugalu mwenye mabao matatu ambayo alifunga kwenye mechi zake tatu
za ligi mfululizo alipoingia uwanjani.
Alianza
kuwafunga Biashara United wakati Simba ikishinda mabao 4-0 Uwanja wa Mkapa na
alifunga bao la pili wakati Simba ikishinda mabao 3-0 Uwanja wa Mkapa na
alifunga bao lake la tatu Uwanja wa Jamhuri Dodoma wakati Simba ikishinda mabao
4-0.
Mugalu amesema:”Ninapenda kufunga ndani ya uwanja na hivyo ndio kazi yangu hivyo nitafunga mabao mengi kila nikipata nafasi ndani ya uwanja na ninafurahi kufunga na nifuraha kwangu kufunga.
"Kikubwa ambacho ninafikiria kwa sasa nikuona kwamba timu yangu inashinda kwanza na mambo mengine yatafuata, nipo hapa Simba ninafurahi hivyo kwanza ninafikiria ushindi wa timu kisha mimi nitafuata na nikifunga mabao zaidi ya 15 nitafurahi," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment