October 7, 2020

 


UONGOZI wa Simba umesema kuwa hauna mamlaka ya kuzungumzia kuhusu kupelekwa mbele mchezo wao wa Ligi Kuu Bara kati yao na Yanga uliotarajiwa awali kuchezwa Oktoba 18.


Leo, Oktoba 7 taarifa rasmi kutoka Bodi ya Ligi Tanzania,(TPLB) imeeleza kuwa mechi hiyo itachezwa Novemba 7 sababu kubwa ikiwa ni uwezekano mkubwa wa kuwepo kwa vikwazo katika usafiri wa kimataifa baada ya kukamilika kwa michezo ya kimataifa iliyopo kwenye kalenda ya FIFA jambo ambalo linaweza kuathiri wachezaji wa vikosi wa timu hizo mbili.

Mchezo huo umepelekwa mbele mpaka Novemba,7 2020, Uwanja wa Mkapa na utachezwa saa 11:00 jioni.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema:-"Simba muda wote tunaamini katika maamuzi ya wenye mamlaka ya mpira siku zote.

"Kila mtu anataka kujua juu ya neno kutoka Simba, sisi tuna msimamo wetu na imani yetu, Klabu ya Simba inaamini katika kile kinachopangwa na wenye mpira.

"Tumekubaliana na tumekubali katika maamuzi yanayofanywa na vyombo, Bodi ya Ligi, Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) sisi muda wote tunaamini katika kile ambacho kinapangwa.

"Yale yanayopangwa na Bodi ya Ligi, Simba haina uwezo wa kupinga mamlaka, wenye mpira wao ni TFF na Bodi ya ligi wao wakiamua sisi hatuna cha kufanya.


"Kazi yetu sisi Simba ni kucheza mpira, hatuhusiki na masuala ya kupanga ratiba hiyo haituhusu sisi, tutafanya kile ambacho tunaambiwa, hatuna kauli na hatuwezi kubadilisha ratiba." 



11 COMMENTS:

  1. Simba haina historia ya ubabe wa kupinga na kulalamika kila kitu. Simba inamheshimu kila mtu na kukubali na kuthamini kila kila la heri na kuiheshimu maamuzi busara ya bodi ya kuendesha mpira na ikihisi kuwa Kuna kitu kimekosewa hainyamazi kimya lakini hushsuriana kwa njia ya heshima kwakuwa Hakuna asiyetenda kosa na hiyo ndio siri ya utulivu na mafanikio kwa Simba

    ReplyDelete
  2. Maamuzi yameegemea upande mmoja jiulize kati ya simba na yanga ni wachezaji gani wa nje walioitwa.Hapo utaona yanga hamna hata mmoja ila simba wapo sasa kwa nini utoe maamuzi yanayomfavour mtu mmoja tukisema tff ni simba msishangae na hii yote ni kwa ajili ya miquissone kwa sababu time yake imepiga kambi ulaya na walijua atachelewa kwa sababu chama,onyango na bwalya nchi zao hakuna restriction

    ReplyDelete
    Replies

    1. BAADA ya Bodi ya Ligi Tanzania, (TBLB) kutangaza kuwa ule mchezo uliokuwa unasubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki wa soka nchini kati ya Yanga na Simba kupelekwa mbele, uongozi wa Yanga umesema kuwa ni jambo jema kwao kujiweka sawa zaidi.
      Taarifa rasmi kutoka TPLB imeeleza kuwa sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kutokana na uwezekano wa wachezaji wa timu hizo mbili kuweza kupata vikwazo vya usafiri kutoka kwenye nchi zao jambo ambalo linaweza kuathiri vikosi vya timu hizo mbili.



      Taarifa imefafanua kwamba kwa sasa nchi nyingi bado zinaendelea kuwa na vikwazo vingi kwenye masuala ya usafiri kutokana na janga la Virusi vya Corona kuendelea kusumbua nchi nyingi.



      Ofisa uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa kwa kufanya hivyo kunatoa fursa kwa timu yao kujiandaa vema zaidi kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa Novemba 7.



      Yanga tayari ilikuwa imeweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo na watani zao wa jadi Simba wanatarajia kuingia kambini, kesho kwa wachezaji ambao hawajaitwa timu ya Taifa.
      Uongozi umefurahi, wewe ni nani hata upinge?

      Delete
  3. Hoja ya kuwepo kwa vikwazo vya usafiri wa anga haina mashiko hata kidogo na inaonesha ni kwa kiasi gani TFF ni wababaishaji kwa sababu kama kigezo cha kusogeza mechi mbele ni vikwazo vya usafiri wa anga iweje hao wachezaji wameweza kuondoka nchini na kwenda huko walikokwenda halafu wakati wa kurudi ndo kuwe kuna vikwazo vya usafiri? Hivi hii inaingia akilini kweli? Hoja hii ni ya kitoto sana na ni watu wachache wenye uwezo mdogo wa kutafakari mambo ndo watakubaliana nayo.Ukweli ni kwamba jambo hili limeamuliwa kisiasa kwa kuegemea kwenye uchaguzi mkuu ili kuondoa attention za watu kwenye kufuatilia matokeo ya uchaguzi mkuu wakati matokeo yakiwa yanafanyiwa ukarabati.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yaani unafikiri hadi tarehe 7 matokeo ya uchaguzi wa tr. 28 yatakuwa bado kutangazwa? Au mimi ndyo sijakuelewa?

      Delete
    2. Ni kweli hujanielewa.....issue sio tarehe ya kutangazwa matokeo,issue ni watu ku concentrate na mechi ya Simba na Yanga,kumbuka matokeo ya uchaguzi hayawezi kutangazwa tarehe 29 au 30,definitely itakuwa ni kuanzia tarehe 31 na kuendelea na kwa wakati huo joto la mechi litakuwa limeanza kupanda maana itakuwa imebaki wiki moja tu mtanange kupigwa..ndugu yangu watu wanajua jinsi gani ya kucheza na saikolojia za watu na kuwatoa kwenye tukio

      Delete
  4. Siasa ya bongo na Afrika nzima ndo kikwazo kikubwa Cha maendeleo ya mpira na michezo yote kwa ujumla.

    ReplyDelete
  5. Siasa ya bongo na Afrika ndo kikwazo kikubwa Cha maendeleo ya mpira nchini

    ReplyDelete
  6. Mzee wa kikosi Kipana tupangie kile kilichoanza na Vitalo au na Morrison Kaitwa Ghana?Maana mlituletea Waha wa Kigoma mkasema Vitalo hacha Morrison awakimbize na mpira wake ukaisha siku ya Bonanza lenu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic