November 25, 2020


 LEO Uwanja wa Azam Complex, Azam FC itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Yanga huku vita kubwa ikiwa ni kwa wachezaji kusaka rekodi mpya ndani ya uwanja.

Kwa upande wa ushambuliaji balaa itakuwa kwa Prince Dube mwenye mabao sita na pasi nne za mabao kati ya 18 yaliyofungwa na Azam FC atakuwa akipambana na Michael Sarpong wa Yanga  mwenye mabao matatu kati ya 13 kwenye kuongeza idadi ya mabao ya kufunga na kuwania kiatu cha ufungaji bora.

Upande wa vita ya walinda mlango ni David Kissu mlinda mlango wa Azam FC vita yake ni kwenye kusaka 'clean sheet' ambapo akiwa amekaa langoni mechi 11 amekusanya 'clean sheet' saba na kufungwa mabao matano kwenye mechi nne na Metacha  Mnata yeye amekaa langoni mechi 10 na kukusanya 'clean sheet' saba na kufungwa mechi tatu.

Safu ya ulinzi ni Bakari Mwamnyeto, safu yake ya ulinzi imeruhusu mabao manne yakiwa ni machache kuliko yale ya Azam FC inayoongozwa na Yakub Mohamed iliyoruhusu mabao matano kwenye mechi 11.


Nyota hawa wawili watakuwa na kazi ya kulinda rekodi zao leo ili kuweka rekodi mpya kwa kuwa ni mara ya kwanza kwa Mwamnyeto kuvaa jezi ya njano akipambana na Yakub kwa kuwa awali alikuwa Coastal Union ya Tanga.

Viungo kwa Azam FC ni mzawa Mudhathir Yahya mwenye pasi moja ya bao ampabo atapambana na Carlos Carlinhos raia wa Angola mwenye mabao mawili na pasi mbili za mabao.

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic