GWIJI wa soka ndani ya Taifa la Argentina ambaye ulimwengu wa mpira unamtambua kutokana na uwezo wake ndani ya uwanja, Diego Maradona amefariki kutokana na mshutuko wa moyo.
Kifo cha nyota huyo kimemkuta ikiwa ni baada ya mwezi mmoja kutimiza umri wa miaka 60 tangu aletwe duniani.
Lengendi huyo mauti yamemkuta akiwa nyumbani kwa mujibu wa mwanasheria wake ikiwa ni wiki tatu zimepita baada ya kufanyiwa upasuaji wa kutoa damu iliyoganda kwenye ubongo wake.
Maradona alishinda taji la Kombe la Dunia mwaka 1986 na alifunga bao ambalo lilipata umaarufu lililoitwa 'bao la mkono wa Mungu' dhidi ya timu ya Taifa ya England na amekuwa ni mfungaji bora wa muda wote ndani ya taifa la Argentina.
Mbali na kuwa mkubwa ndani ya uwanja kwa wachezaji wote nje ya uwanja alikuwa akifanya vituko kutokana na masuala ya kujihusisha na matumizi ya pombe pamoja na kuwa kwenye ishu ya matumizi ya madawa ya kulevya jambo ambalo linatajwa kushusha kiwango chake zama alipokuwa anacheza.
Rais wa Argentina, Alberto Fernandez ametangaza siku tatu za maombolezo baada ya kupata taarifa za kifo cha Legendi huyo .
" Ulitufanya tukawa guzo kwenye dunia umefanya yale yasiyofikirika kutokea ulikuwa ni bora muda wote, asante kwa kuwa uliweza kuja Diego tutakukumbuka muda wote," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment